hello!
mrejesho.
Lile tatizo nashukuru Mungu limeisha sasa niko vizuri.
ila wakati mnanishauri kuna waliosema kuwa nampenda sana mwanaume wangu ndio imepelekea saikolojia yangu kuwa vile.
sasa tiba niliojipa ni kuchange mind
ninapotaka kumuwaza yule mwanaume nawazia vitu vingine
japo ilikua ngumu ila niliweza baada ya kuona anazidi kunisababishia matatizo
nikaanza kumtoa moyoni..
nikaweza.
sasa baadaya ya kumtoa nikaanza kumuona wa kawaida feeling nae hata kukaa nae naona uvivu
yani mwanzo alikua ananitetemesha nikimkosea
lakini nmekua sina hofu nae kabisa..
mpaka nafikia hatua ya kuona its ok hata tukiachana yani amenitoka moyoni..
sasa najiuliza ni kawaida mtu kumtoa moyoni namna hii
halafu kusema nimpende tena moyo umekua mzitoo..
je ni kawaida? au tiba ya saikolojia niliojipa iliniathiri?
maana niliona yeye ndo chanzo cha yote!