Msaada haraka Chanjo ya manjano(yellow fever) nataka kusafiri nje ya nchi

G-stev

Member
Joined
Aug 24, 2020
Posts
13
Reaction score
10
Habari wana jamii, samahani ndugu yenu nimepata safari nnje ya nchi sasa sijui chanjo ya manjano inachukua mda gani kudungwa dosi na kupata cheti chake maana safari ipo karibu sana. Naombeni msaada kwa wazoefu tafadhali
 
Habari ndugu. Nijuavyo mimi, kama upo Dar, hospitali ya mnazi mmoja pale ndo walikuwa wanatoa hiyo chanjo.
Haina mambo mengi, unaenda na Passport yako unasema unataka chanjo ya manjano.

Utapewa chanjo hapo hapo na cheti kinatolewa muda huo huo. Sina uhakika sana ila nadhali huduma hiyo wanatoa kila Jumanne.

Chanjo yenyewe ilikuwa inatolewa kwa shilingi elfu tano enzi hizo. Mimi nilipewa nadhani mwaka 2009, lazima kutakuwa na mabadiliko mengi.
 
Bongo land....😁
1000011170.jpg
 
Sasa hivi ni 30,000/= na haina ku renew kama zamani.
 
Attachments

  • IMG_4060.jpeg
    IMG_4060.jpeg
    1.3 MB · Views: 37
Habari ndugu. Nijuavyo mimi, kama upo Dar, hospitali ya mnazi mmoja pale ndo walikuwa wanatoa hiyo chanjo.
Haina mambo mengi, unaenda na Passport yako unasema unataka chanjo ya manjano.

Utapewa chanjo hapo hapo na cheti kinatolewa muda huo huo. Sina uhakika sana ila nadhali huduma hiyo wanatoa kila Jumanne.

Chanjo yenyewe ilikuwa inatolewa kwa shilingi elfu tano enzi hizo. Mimi nilipewa nadhani mwaka 2009, lazima kutakuwa na mabadiliko mengi.
Ni sahihi
Ila aende asubuh
 
Inawezekna kwa mtu kutoka nje akiwa anakuja hapa nchini kupata hii chanjo au tukafoji certificate yake tuuu
 
Mkuu hii imekaaje?? Kama nataka certificate yake tu kwa raia wa kigeni
Kipindi cha nyuma kulikuwa na jamaa wanakupa hiyo kadi kwa elfu kumi. Inakuwa imegongwa muhuri na kila kitu ila sidhani kama bado wanafanya ile ishu.
 
Yellow fever ipo usinunue cheti kwenye afya yako utakuja kusumbuka baadae kama ni msafiri...
 
Inawezekana. Yangu Ilikuwa ya ku renew kila baada ya miaka kumi.
Kwa sasa lazima hiyo 30,000/= ulipie zile janja janja za zamani hakuna, na moja kwa moja utaingia ktk system ,
 
Back
Top Bottom