MSAADA, HASWA KUTOKA KWA WATUNZA KUMBUKUMBU WA SIMBA.

JOTO LA MOTO

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2018
Posts
758
Reaction score
555
Kipindi nakuwa nilitokea kuwa mnazi kindakindaki wa timu ya Simba, ingawa kwa sasa sio kwa asilimia zile zile nilizokuwa nazo kipindi kile. Wakati ule nilitokea kuvutiwa na baadhi ya Majina ya Wachezaji kadhaa, hivyo basi ombi langu naomba yeyote mwenye taarifa walipo Jamaa hawa kwa sasa, na kama walishatangulia mbele ya haki basi Wapumzike kwa amani. Wachezaji hawa wafuatao:- Sunday Juma, Zuberi Magoha, Lila Shomari, Malota Soma, Ezekiel Grayson (Jujuman) huyu nilisikia baadae kwamba ndiye Baba wa Aunty Ezekiel, Kiwelu Musa, Moses Mkandawile, Ibrahim Marekano, Abdul Mashine, Daudi Salum (Bruce lee)...
 
Musa Kiwelu ana undugu na Jamuhuri Kiwelu?
 
Namkumbuka Zuber Magoha tangu akicheza Jumuiya ya Arusha miaka ya nyuma kabla ajaenda Simba.Alikuwa ni mchezaji wa miraba minne,nguvu,kasi,mishuti mikali na chenga nyingi.
 
Jina la utani la Zuberi Magoha lilikuwa lipi?
 
Musa Kiwelu ana undugu na Jamuhuri Kiwelu?
Ndio ni Kaka yake wengine ni Mhesa Kihwelo, Mhehe Kihwelo na Kihwelo mwingine alichezea Yanga. Wote ni waliwahi kucheza mpira tena Ligi Daraja la Kwanza au Ligi Kuu kwa sasa.
 
Mwanamtwa Kihwelo a.k.a Dally Kimoko Kiraka
 
Namkumbuka Zuber Magoha tangu akicheza Jumuiya ya Arusha miaka ya nyuma kabla ajaenda Simba.Alikuwa ni mchezaji wa miraba minne,nguvu,kasi,mishuti mikali na chenga nyingi.
Zuberi na Mogela walikuwa Watesi wazuri kwa mabeki wa timu pinzani.
 
Ndio ni Kaka yake wengine ni Mhesa Kihwelo, Mhehe Kihwelo na Kihwelo mwingine alichezea Yanga. Wote ni waliwahi kucheza mpira tena Ligi Daraja la Kwanza au Ligi Kuu kwa sasa.
Musa yeye yu wapi kwa sasa?, maana namuona Jamuhuri ndiye anatamba kwenye media.
 
Kipindi nakuwa nilitokea kuwa mnazi kindakindaki wa timu ya Simba, ingawa kwa sasa sio kwa asilimia zile zile nilizokuwa nazo kipindi kile. Wakati ule nilitokea kuvutiwa na baadhi ya Majina ya Wachezaji kadhaa, hivyo basi ombi langu naomba yeyote mwenye taarifa walipo Jamaa hawa kwa sasa, na kama walishatangulia mbele ya haki basi Wapumzike kwa amani. Wachezaji hawa wafuatao:- Sunday Juma, Zuberi Magoha, Lila Shomari, Malota Soma, Ezekiel Grayson (Jujuman) huyu nilisikia baadae kwamba ndiye Baba wa Aunty Ezekiel, Kiwelu Musa, Moses Mkandawile, Ibrahim Marekano, Abdul Mashine, Daudi Salum (Bruce lee)...
Sunday Juma alitokea timu mmoja ya Mkoa wa Kilimanjaro nadhani ni Kibo Shooting au Ushirka FC na alikua winga wa kulia akiwa na mbio sana na pale Msimbazi akipewa jina la utani la "kiberenge" kutokana na kasi yake kama mkimbiaji wa mbio fupi vile. Huyu sijui yupo wapi siku hizi

Zuberi Magoha (center forward), Lila Somari (half back four), Ibrahimu Marekano(holding midfilder), Super Kiwelu Musa(full back wright), Moses Mkandawile(goalie), na Eekiel Grayson "Jujuman(attacking midfielder) walishatanguli mbele ya haki

Huyu Jujuman ambaye ndio Baba yake msanii wa Bongo Movie Aunt Ezekiel yeye alicheza mpira nyuma kidogo ya hao wengine. Alicheza na kina Jummanne Hassan "Masment', Mohamed Kajole "Machela", Daud Salum "Bruce Lee",Mohammed Bakari "Tall" Kipa Omar Mahadh Bin Jabir, Thuweni Ally na George Kulagwa, kuwataja wachache

Sunday Juma alikuja baada ya hapo na kizazi chake ni kina Mtemi Ramadhani, Idi Pazi (kabda hajaenda Sudan kucheza soka ya kulipwa) na miaka ya mwanzo ya Mogella Zamoyoni

Malota Soma(Ball Juggler) kama alivyosema mdau mmoja yupo maeneo ya Magomeni Usalama akiendesha taxi yake. Ama kina Abdul Mashine, na Daud Salum sina taarifa zao
 
Shukran za dhati Mdau kwa taarifa hii muhimu.

Wapate Pumziko la Amani waliotutangulia mbele ya haki.

Nafahamu fika kuwa nimechanganya vipindi tofauti hapo, ila hayo ni kati ya Majina yaliyonivutia na kunasa kichwani kwangu kwa muda wote nilipokuwa mfuatiliaji kindakindaki wa Wana Msimbazi.

Sunday Juma nakumbuka aliitwa' Pikipiki' sina uhakika sana na hilo la Kiberenge, sikulisikia sana.

Lila Shomari alikuwa na Ndugu yake Allan, ila nakumbuka yeye alikuwa Yanga kama sikosei, naye yu wapi kwa sasa?
 
Nimewataja hao lakini haimaanishi nimemsahau 'Golden Boy' Zamoyoni Mogela, la hasha..ni kwamba Zamoyoni nimefanikiwa kumuona na kupata habari zake mara kadhaa.

Zamoyoni anabaki kuwa namba moja kwenye listi yangu.

Hao wengine ndio sikubahatika.
 
Back
Top Bottom