Msaada: Hatua za kuachana na mume wa ndoa

Msaada: Hatua za kuachana na mume wa ndoa

Naboti

Senior Member
Joined
Apr 17, 2015
Posts
189
Reaction score
48
Wataalamu naomba mnisaidie nina tatizo la ndoa,

Ndoa hii ni ya kikristo ina miaka sita kwa sasa lakini imekuwa na makelele mengi kila kukicha, tumeshatengana mara kadhaa na kusuluhishwa lakini kwa sasa hivi tunaishi tu kama mtu na adui yake ndani ya nyumba moja.

Watu wa nje wanadhani ni ndoa kumbe hamna kitu ni kuwaridhisha tu wale waamuzi kama mchungaji na washauri wa ndoa.

Mimi kwa upande wangu kama mwanamke siridhishwi kuishi na mwanaume ambaye haonyeshi kunipenda kiasi cha kuishi tu kama mtu na adui yake kwa nje watu watuone tuko pamija wakati rohoni kila mtu na mwenendo wake.

Nafikiria kutafuta talaka katika vyombo vya sheria lakini sijua nianzie wapi wala nimalizie wapi wala iweje.

Naomba msaada kwa wanaojua
 
Mhh ngoja wataalam waje wakupe ushauri mkuu ila mna watoto?
 
Msiachane, kaeni pamoja muangalie tatizo lilianzia wapi, then muanze kurekebisha kuanzia hapo. Anza kujishusha wewe kwanza, jifanye tu kama mjinga umuombe msamaha hata kama unajua huna kosa. Hebu anzia hapo kwanza alafu mengine yatafuata
 
Mama miye ni msajili wa ndoa za Kikristo. Nimewahi kukutana na wengine ka weye. Ushauri wangu ni huu; Huna pa kwenda tena!! Sijui ka utaniamini ila huo ndo ukweli kabisa wa ndoa ya Kikristo. Nadhani umewahi kusoma maandiko haya; Marko 10 : 9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
Swali langu ni kwamba, Je ulikurupuka kuingia katika ndoa hiyo? Ulishurutishwa? Una uhakika gani kwamba mwenye tatizo sio wewe ni yeye?
Ushauri wangu; Acha kiburi, nyenyekea chini ya mumeo, sikiliza mashauri ya wakuu, mlilie Mungu zaidi kuliko kuwalilia watu. Kiila mtu, anayo mizigo yake. Nyumba nyingi leo hii zipo ICU, usitamani ya mwingine. Chezea yako mpaka uikute jehanam.
Kwa faida ya wale wenye mawazo ka yako; Ndoa ya Kikristo hainaga talaka. Mpaka kifo kiwatenganishe
 
Kama tatizo la ndoa sio zinaa sikushauri kuachana naye lakini unaweza kuanzia TAWLA ukapata msaada wa kisheria zaidi. Kila la kheri
 
Mkuu mangatara,maelezo yako na ushauri wako ni mzuri sana...hali hii inatokana na wengi kuingia ndoani kama fashion,kwamba fulani kaowa/olewa ngoja na mimi nichangamke nisichelewe,kumbe hawajui hasa kinachowapeleka kwenye tendo lenyewe na wakikutana na misukosuko kama hii badala wamwombe Mungu awaonyeshe njia wanakimbilia kuachana..pia watu maandiko matakatifu hawayasomi hata kama wanayasoma may be hawayaelewi ndo maana unakuta mtu kwa sababu haelewi maana halisi ya ndoa akila chakula chumvi imezidi kidogo anatishia kutoa talaka,huku mwanamke ameona mume kasimama na mfanyakazi mwwnzie anataka talaka..dada Naboti kama mlifikia kungia Kanisani mkala kiapo there's no way out usubiri Mungu amchukue mumeo au utangulie wewe hakuna zaidi ya hapo,muhimu kaeni chini myaongee haya maswala hakuna popote duniani watu wakaishi bila kupishana lugha ila kama ulimfumania live anazini basi ni haki yako.
 
Last edited by a moderator:
Khantwe title inasema "naomba msaada",hata ushauri ni msaada so wenye kutoa msaada wanaweza'angalia na kupima tatizo na hapo amepewa msaada wa kukumbushwa viapo alivyoapa..
 
Last edited by a moderator:
Khantwe title inasema "naomba msaada",hata ushauri ni msaada so wenye kutoa msaada wanaweza'angalia na kupima tatizo na hapo amepewa msaada wa kukumbushwa viapo alivyoapa..

[h=2]Msaada wa Hatua za kuachana na mume wa ndoa[/h]Mmmmhhh...hivi eeh?
 
Beba mizigo yako na unachoona cha thamani kwako then ondoka.
Ukiwahusisha wazee wa kanisa tegemea mahubiri upya.
 
Mama miye ni msajili wa ndoa za Kikristo. Nimewahi kukutana na wengine ka weye. Ushauri wangu ni huu; Huna pa kwenda tena!! Sijui ka utaniamini ila huo ndo ukweli kabisa wa ndoa ya Kikristo. Nadhani umewahi kusoma maandiko haya; Marko 10 : 9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
Swali langu ni kwamba, Je ulikurupuka kuingia katika ndoa hiyo? Ulishurutishwa? Una uhakika gani kwamba mwenye tatizo sio wewe ni yeye?
Ushauri wangu; Acha kiburi, nyenyekea chini ya mumeo, sikiliza mashauri ya wakuu, mlilie Mungu zaidi kuliko kuwalilia watu. Kiila mtu, anayo mizigo yake. Nyumba nyingi leo hii zipo ICU, usitamani ya mwingine. Chezea yako mpaka uikute jehanam.
Kwa faida ya wale wenye mawazo ka yako; Ndoa ya Kikristo hainaga talaka. Mpaka kifo kiwatenganishe

Acha kuongopa na kupotosha, ndoa ya kikristo inavunjwa kama ndoa nyingine tu zinavyovunjwa, na kwa ukristo kama mmoja ametembea nje ya ndoa na kuna ushahidi hilo sababu kubwa ya kuvunja ndoa na inavunjwa kikanisa kabisa, hivyo acha kumdanganya na kumfanya aishi maishi ya shida wakati kuna uwezo wa kuachana!

Hakuna msamaha mmoja anapotembea nje ya ndoa!
 
Yeah Khantwe....wangeweza kumwambia aende mahakamani na angeweza kufanikiwa but vipi kuhusu nafsi yake na yale aliyoyaapia,alimdanganya Mungu wake sio?maana kwa imani anayoiamini si ruhusa mwanandoa kuomba/toa talaka.
 
Last edited by a moderator:
Barbarosa acha kumshambulia jamaa hajaongopa wala kupotosha/japo ni kweli uliyoandika,ktk hili bandiko hakuna palipoandikwa kwamba alimfumania huyo mumewe akizini mangatara alimshauri kulingana na kile alichoki-post humu yeye siyo mnajimu amshauri kana kwamba ameoteshwa matatizo ya huyo mama.huyo dada aje hapa atoe sababu zinazopelekea kutaka talaka uone atakavyomshauri kwa mara nyengine.
 
Last edited by a moderator:
Katafute shauri lililowahi kufunguliwa mahakamani kwa jina la MARIAMU TUMBO V. HAROLD TUMBO,ukiisoma hii kesi ya ndoa yote mpk ukaimaliza utakuwa ushajua nn cha kufanya na sababu zipi za kuiiambia mahakama ili ikupatie iyo decree of divorce!hii kesi maelezo yake/facts inafanana kidogo na yako,so itakuwa ni marejeo mazuri tu kwa shauri lako.

Ila kwa ufupi jambo lako linawezekana kabisa kwa mujibu wa sheria za ndoa za Tanzania. Ila ni vyema kwanza ukaanzia katika bodi ya usuluhishi wa ndoa,ikishindikana kusuluhisha mgogoro wenu then unafungua petition/ombi mahakamani ili upatiwe talaka kutokana na amri ya mahakama lakini lazima uithibitishie mahakama kwamba ndoa yenu imevunjuka bila uwezo wa kutengemaa tena/irreparably broken down.
 
Ndugu heri ukosee kujenga ila sio kuolewa, kumbuka ndoa ndio maisha ya hadi kifo, kama huna amani basi utakua hivo hadi kifo.

Pokea ushauri chambua sema na moyo wako.

Taratibu anzia ngazi ya familia
 
Duuh! Ndoa ya kikristo haivunjikagi kirahisi ivyo! Grounds za kuvunja ndoa ya kikiristo ni mpaka utafute ushahidi pasi na shaka kuwa mumeo sio muaminifu kwa ndoa yenu!
 
Back
Top Bottom