Msaada hatua za kufuata ili kubadili jina kisheria

Sawa.
 
Deed Poll Ni nini?

Ni nyaraka ya kisheria inayotumika kubadilisha jina la mtu. Nyaraka hii hua inasainiwa na mtu ambaye anabadilisha jina pekee tofauti na nyaraka nyingine za kisheria ambazo zinasainiwa na watu wawili mfano Mikataba. Nyaraka hii kwa kawaida inashuhudiwa na kamishna wa viapo ambae ni hakimu au wakili.

Kwa nini Ubadilishe Jina?

Kisheria huwa ni halali mtu kubadilisha jina. Na baadhi ya sababu za kubadilisha jina zinaweza zikawa kama ifuatavyo:

1. Ndoa-Mtu ameolewa anataka achukue jina la mwisho la mke au mume wake.

2. Dini- Mtu amebadilisha dini ikapelekea kubadilisha jina lake.

3. Ulikua unatumia majina matatu mfano Jua Kali Halishi ukataka utumie majina mawili tu Jua Halishi

4.
Kuna mkanganyiko wa majina kwenye nyaraka zako za kudumu mfano jina la kwenye cheti cha kuzaliwa ni tofauti na la kwenye cheti cha shule.

5. Nakadhalika.

Ufanyeje ili mabadilisho yako ya jina yatambulike kisheria?

Unatakiwa uwape(ule kiapo) kwa kutumia deed poll (nyaraka ya kubadilishia jina). Hivyo basi fika kwa hakimu au wakili yoyote ataandaa nyaraka hii kwa kumpa taarifa zako mwisho utatia sahihi yako na wakili au hakimu atashuhudia na kugonga muhuri wake kwenye deed poll aliyoiandaa kwa ajili yako.

Baada ya kupata deed poll ufanyaje?

Kwa mujibu wa sheria, deed poll inatakiwa isajiliwe na msajili wa nyara
ka ili iwe halali na uweze kuitumia sehemu mbalimbali mfano kwenye maombi ya passport, kuomba mkopo, kazi, mafao ya kustaafu nk. Hivyo Basi baada ya kupata deed poll yako unatakiwa uipeleke kwa msajili wa nyaraka (registrar of documents) ili iweze kusajiliwa na kutambulika katika matumizi mbalimbali

Maelezo haya nimeyachukua kwa tabibumtaratibu kwani ni maelezo yanafanana na niliyotaka kuyaleta hapa. Vilevile mada hii ilishawahi kujadiliwa

GODZILLA mFuKuZa nDoTo City Accountax Associates

Mifano hii ya Deed Poll ni ya kwangu

View attachment 1692356View attachment 1692357
 
Shukrani bosi
 
Nami niliwahi kufanya marekebisho ya jina langu na huu ndio ulikuwa utaratibu nioioufuata 2016..
So mjumbe fuata ushauri huu
 
Marehemu Mobutu Seseseko wa Congo angekuwa hai angekuelimisha zaidi . Kama umefanikiwa kuachana na imani za kizungu nakupongeza . Kubadili jina ni yatua tu za kisheria

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…