Uko sahihi ni Lactation Amenorrhea. Hutumika kama njia ya uzazi wa mpango kwa uhakika kwa miezi sita ya mwanzo mara baada ya kujifungua. Baada ya hapo ni vyema ukatumia njia nyengine ya kupanga uzazi hata kama bado hujapata hedhi maana inakuwa sio njia ya kuaminika tena.Wakati wa kunyonyesha hormone ya prolactin inakuwa juu sana hivyo kuzuia upevushaji wa mayai, ndiyo maana unakosa hedhi. Wengine huwanyonyesha watoto wao kwa muda mrefu na Mara kwa Mara kama njia ya uzazi wa mpango. ( sio Doctor nimejibu kutokana na uelewa, kama kutakuwa na hitilafu doctors watarekebisha)