Msaada: HIV Non reactive

Pole Mkuu, hapo ni suala la elimu ya upimaji tu. Non reactive maana yake, Probably huna Virusi vya UKIMWI. PROBABLY. Ili kuwa na uhakika zaid pima tena baada ya miezi mitatu(angalizo: usipige tena kavu ndani ya hiyo miezi).

Changu huwa kinasoma kwenye C. Namshukuru Mungu kwa hilo.
Maaaaaaaaaaaana................
 
Kwa baadhi ya maelezo ya wadau hapa antibodies ni kingamwili, hii ina maana antibodies ni walinzi wa miili yetu dhidi ya mashambulizi ya uambukizo wa magonjwa mbalimbali.
Hao walinzi wakiwa imara/wapo active yaani positive, maana yake ulinzi wa mwili ni imara.
Swali inakujaje mtu mwenye ulinzi imara yaani antibodies positive akawa tena muathirika eti HIV POSITIVE? Wakati ulinzi au kinga ya mwili wake ni imara?
Kuna nini nyuma ya pazia hili la HIV na PHAMACEUTICAL INDUSTRIES?
Au za kuambiwa tuchanganye na zetu?
 
Kipimo kilichotumika ni reaction kati ya "antibody" na "antigen",,so kama ni reaction jibu litakua ni either reactive or non reactive
 
Antibodies ziko specific kwa antigen(intruder) so huzalishwa pale specific antigen anapokuepo(mwili unapogundu) mwilini,mfano HIV(Antigen),antibodies agaist HIV zitategenezwa pale mwili utakapogundua kuwa yupo,maradhi hutokea pale hizo kinga mwili zinapozidiwa na hao intruders(antigen).

Nimetumia lugha rahisi sana
 

we ni muongo sana!muache elimu zenu za kimagharibi kukaririshwa hovyo bila hats kujiongeza!

je unajua kuwa H.I.V alikuwepo toka miaka ya 1930s?sasa kwanini babu zetu hawakuteseka na hili gonjwa?

unajua ni kwanini nchi zilizo chini ya jangwa LA sahara zina maambukizi makubwa ya H.I.V ukilingsnisha na nchi za ulaya?
 
Andika huo ukweli basi ambao ni elimu ya mashariki I don't know kusini
 
Non reactive haina tofauti saana na negative kihalisia bali ni lugha tu. None = Hakuna, reactive ni mabadiliko yanayopatikana baada ya antibody kuungana na it's specific antigen na kutoa mabadiliko ambayo hutambuliwa kitaalam. Sababu ya kukutoa haina maana ya kukupa majibu mabaya sema tatizo ni ufupi wa muda uliotumika ambao kwa uchache cyo chibi ya dk 10 lakn hyo ya dk 3 na 5 SOP ya HIV tesring haiko hvyo. So, majibu yako yamepima miezi mitatu kurudi nyuma na cyo umefanya nn chini ya mwezi. Msaada wangu kwako badili tabia yako ya mahusiani cyo nzuri, KWA NINI ucjiamini iwapo huna pitapita zenye mashaka? Baki barabara kuu ndg yangu acha michepuko!!
 
Nyinyi huko muna raha munapima bure hayo magonjwa mimi huku Ughaibuni kupima ni kwa Pesa Dollar 500$ sawa na shilingi Milioni 1 na laki 1 mara ya mwisho nimepima mwaka 2011 na nikawa nipo HIV Negative Hepatitit B Virus, TB, Cancer, Tezi dume vyote hivyo vipo poa nitakwenda tena kupima baada ya kumalizika mwezi wa Ramadhani mwezi wa 7 mwaka huu. Laiti ningekuwa niko bongo ningekuwa ninapima kila baada ya miezi 6.
 
Mkuu upo kijiji gani wewe? kama upo karibu na kijiji cha kondoa irangi mjini dodoma nifahamishe hao wanaopima watakuwepo mpaka lini? kwani nina mteja wangu ana HIV Positive yupo huko kijijini kondoa ninataka akapime kwani nina mtibia sasa mwezi ni 3 na anaendelea vizuri kiafya. Sasa sijuwi hao wapimaji wa AMREF watapita huko kijijini kondoa irangi? Au hawapo sehemu hizo?
 
Pole Ndugu yangu. Hongera kwa kufanya maamuzi mazuri ya kupima. Kuna comments nyingi zimetolewa zinging ni Kwesigabo
 
Nilikuwa sijamaliza. Comments zingize ni saw a. Lakini zingize ni uongo au si za kiungwana. Kama walivyosema baadhi, majibu yako ni mazuri. Huna dalili za kibiologia kuwa umeshapata maambuki ya VVU. Ili uwe na uhakika kuwa hujapata maambukizi ya VVU usifanye ngono zembe kwa miezi 3. Baada ya miezi 3 kapime tena. Kama majibu yatakuwa non-reactive basi utakuwa na uhakika. Mimi sijatumia neno Ukimwi kwa sababu Ukimwi unaonekana miaka 7-10 baada ya kupata maambukizi ya VVU
 
Mkuu isikusumbue hiyo ni jinsi tu ya kutoa jibu na kurecord ilikuwa hivi ilikuwa inaandikwa positive na negative kila mtu akajua maana yake hivyo wale positive wakajiona kama mtu akiona kadi yake anamjua ni ana maambukizi hasa kwa wale wajawazito kwenye kadi ya klinik wakajinyanyapaa wakawa wanakwepa kupima majipu yakabadilshwa yakaingizwa kwenye kizungu kikali zaidi reactive maana yake imejitokeza na non reactive haijajitokeza ili awe anaejua ni aliyepima na aliyepimwa bado kuna watu wachokonoaji wakajua hivyo litabadilishwa tena maana iliandikwa pia pmtct 2 huyu hana pmtct 1 anayo wakajua akiona ana 1 anaibadili kuwa 2 au wengine wanatafuta kadi nyingine wanakopi wanaweka 2 ni shida kwa kweli ila amini jibu utakalopewa na mpimaji na siku hizi utaalamu umekuwa ukipima mara ya kwanza ukawa huna huna haja ya kupima tena usubiri mwaka mmoja siyo miezi 3 tena endelea kuwa mwaminifu au tumia kondom ndg yangu ARV zina shida sana mwilini
 
Maswala ya window period nayajua mkuu. Shida yangu sio kujua hayo. Nlitaka kujuankma Nn Reactive = Negative bhaaasiiii. Haijalishi ni negative au non reactive suala la window period liko pale pale kama umepata maambukizi ya karibuni. Otherwise asante kwa mchanganuo wako kiongozi
 
Boss nashani umeshauri jambo usilokuwa na elimu nalo kulitaalamu. Naoa unatumia unayoyawaza wewe. Pole ya nini? Mi nia HIV?? Non reactive means Negative. Mtumie hata gpogle akusaidie sio kupanikisha watu
 
Boss nashani umeshauri jambo usilokuwa na elimu nalo kulitaalamu. Naoa unatumia unayoyawaza wewe. Pole ya nini? Mi nia HIV?? Non reactive means Negative. Mtumie hata gpogle akusaidie sio kupanikisha watu
Anachosema ni kwamba kipimo kimoja cha HIV hakiwezi kuwa conclusive.

Ukipata maambukizi leo na kwenda kupima kesho virusi vinaweza visionekane kwenye vipimo kwa sababu idadi ya virusi ni ndogo sana.

Ndiyo maana kuna ushauri wa kuacha kabisa risky behavior na kwenda kupima tena baada ya miezi mitatu. Kwa sababu baada ya miezi mitatu kama ulikuwa na virusi hata vichache sana vina nafasi kubwa ya kupimika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…