Mkuu
Shoo Gap,
'Check up'...esp. Full body check up ni (Body scan kuangalia magonjwa au uwezekano wa magonjwa) na tunaisistiza angalau mara moja kwa miezi mitatu.Hii tukimaanisha uchunguzi wa afya kufanyika kwa karibu kila kiungo.
Mwilini kuna baadhi ya sample tunazozitumia kuangalia vitu/mambo mbali mbali katika kuangalia, kuchunguza, kufuatilia/kuangalia maendeleo ya mgonjwa(patient) au client(iwapo haumwi).
Ikumbukwe wengi wa watu wanaokwenda hospitalini huenda kama Patients na siyo Clients.
Sasa katika mwili wa binadamu tunaweza kuangalia haya yafuatayo(HAYA ni BAADHI TU.)
Damu:
-Kundi la damu,
-Sukari
-Madini(Na, K, Ca, Cl)
-Wingi wa damu
-Chembe chembe za damu, nyeupe, sahani n.k
-Urea
-Creatinine
-Mafuta yaliyo mwilini(Lipid Profile)
-Homa ya ini(Hepatitis Panel)
-VVU
Mkojo:
-Sukari
-Chembe za damu (nyeupe, nyekundu)
-Protini
Choo:
-Mayai ya minyoo
-Damu
CSF:
-Protini
-Chembe nyeupe za damu
Upigaji picha:
-Picha ya kifua((X-ray)/ CXR
-Picha ya moyo(ECG, ECHO)
-Uchunguzi wa masikio, pua na kinywa.
Kwa wanawake kuna vitu vingine kama;
- Abd-Pelvic USS/ Obstetric USS
- Pap smear n.k
Kila kipimo kina gharama yake, na hivyo basi watu kusita kufanya vipimo hivyo, Sasa ni jukumu la daktari wakati fulani kwa kutumia elimu yake kuangalia vipimo vipi avipe vipaumbele kuliko vingine, na hivyo basi SIJAONA kosa hata kidogo pale daktari alipokuambia ukatoe damu, mkojo n.k.