Msaada: Huu mlio wa usukani “sterling “ya gari nikapaki gari kwa muda eneo lenye baridi

Bakulutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2011
Posts
2,557
Reaction score
1,787
Nikipaki eneo lenye baridi kama masaa 4 nikiwasha gari nikiwa na zungusha usukani ina lalamika ngiiiiiii nikirudi upande wa pili hivyo hivyo . Inabidi niache gari ingume kama dk 10 mpaka 15 ndio unapotea.

Tatizo linaweza kuwa nini? Mwaka hana ilikuwa hivyo hivyo nilipo kuwa huko kijijini. Ila jana nimepaki mahali hapa mjini kuna baridi haswa jioni ile naona imelalamika saana inabidi nisubirie kwa muda.
 
We jamaa una gari kumbe? Ni aina gani, ya mwaka gani, baridi nyuzijoto ngapi?
 
Ndio maana unashauriwa kuwa asubuhi ukiamka washa gari kisha iache iungurume dk 10 mpaka 15 ili oil isambae sehemu husika na pia kuondoa barafu (if any).
 
Ndio maana unashauriwa kuwa asubuhi ukiamka washa gari kisha iache iungurume dk 10 mpaka 15 ili oil isambae sehemu husika na pia kuondoa barafu (if any).

Hii ni muhimu sana ila kwa hii issue ya uskani inachukua muda sana kupotea.
 
Si upeleke kwa mafundi mkuu!
Siyo mafundi wa vichochoroni, halafu upo mji gani mzee wenye baridi, njombe au!?

Fundi wangu naemuamini hapa mjini nilimuuliza nikaona ana mashaka mashaka kama hana uhakika fulani na nifundi wa kuaminiwa wa Subaru hapa Dar es Salaam.

Hakuna fundi wa uchochori anaegusa hii gari bora ni paki kama fundi wa maana wako busy. Muhimu hapa nataka kujua ni tatizo au nikawaida? Wakati fulani JF pia kuna watu wanajua vitu vingi sana unaweza pata idea kabla hata fundi hajagusa gari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…