Msaada: Huu ni ugonjwa gani kwa kuku?

Msaada: Huu ni ugonjwa gani kwa kuku?

Chuck j

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2011
Posts
2,366
Reaction score
828
wanajamii habari zenu,
Ninafuga kuku, tatizo limejitokeza tangu Jumamosi, kuna kuku 1 anachechemea, nimejaribu kumchunguza labda anakidonda au kapigwa but hakuna, kuku ana umri wa miezi 6 wenzake wanataga ilayeye hata kupandwa hataki. Sijui ni ugonjwa gani umemfanya akachechemea.
 
Anachechemea.......!!! Ungetoa na dalili nyingine ambazo si za kawaida. Hapo itakuwa ngumu kujua ni ugonjwa gani hasa.
 
analala muda mwingi,na kingine kuku mwingine akiwa anampiga anasimamisha manyoya ya kichwani. hayo tuu,kula anakula vzr tuu.
 
analala muda mwingi,na kingine kuku mwingine akiwa anampiga anasimamisha manyoya ya kichwani. hayo tuu,kula anakula vzr tuu.

Analala muda mwingi ana mdondo????

Wakati wa kupigana ni jambo la kawaida kwa kuku kusimamisha manyoya ya kichwani hadi shingoni

Kinyesi chake kikoje?
Macho?
Mabawa yako kawaida au kayashusha na yamenyambuka flani hivi???

Chunguza hao kuku vizuri
Ukishindwa wape majani ya mgagani (hiyo sio tiba ni huduma ya kwanza tu)
 
Huenda pia ni mojawapo wa madhara ya kupandwa, jogoo amekuwa mzito kwako na amemtengua mguu
 
Back
Top Bottom