msaada huyu naye ana mapenzi au...


asante ila sasa mambo yanakuwa magumu, mtoa ushauri naanza kuogopa sikuwa na hilo wazo kabisaaaa, sasa MGONJWA atatuelewa tukimwambia awaone washauri nasaha!!! si anaweza kutuambia sisi ndio wagonjwa maana hapa yanakuja yale ya boss kuambiwa ana minyoo!!
asante nitajitahidi kufikiria jinsi ya kufikisha ujumbe kwa shoga naendelea kupokea ushauri nijue nini haswa nikamshauri!!
 
Huyo 'kijana' ana tatizo la akili linaitwa OBSESSION.

Umeona movie ya Beyonce? Obsessed?

asante sikuwa naufahamu huu ugonjwa nime-google, kweli JF home of great thinkers, thanks!!
 

Sio ngumu, mwambie amjaribu. Kwa ugonjwa alionao (Obsessive Compulsive Disorder - OCD), inatakiwa mshauri/mshauri nasaha afanye angalau vifuatavyo:

  • Kumshawishi huyo kaka aamini kwamba lengo lake (goal) la kuwa na huyo dada kama mke haliwezi kutimia (it is impossible to meet the goal).
  • Aamini kuwa kuendelea kufikiria kwamba lengo lake linaweza kutimia is irrational and unreasonable given his circumstances.
  • Aamini kuwa si lazima kufikia malengo ambayo yapo nje ya uwezo wake. Ajifunze ku settle for lesser but satisfying goals ambazo zipo ndani ya uwezo wake.
Pia jaribu kumwambia rafiki yako awe very clear kwenye kauli zake kwa huyo kaka kwa sababu inawezekana naye pia anachangia kulikuza tatizo kama anatoa majibu ambayo yanamfanya huyo kaka aamini kwamba iko siku moja wanaweza kuwa pamoja. Kama hampendi, ni vizuri aliweke hili very clear kwa macho makavu kabisa na bila kuuma maneno!
 

Asante! nitajitahidi kufikisha ujumbe na kuyatekeleza hayo kwa makini zaidi, kama kutafuta mshauri mwenye utaalam huo ili atusaidia kufikisha ujumbe,
kuhusu huyu rafiki kuwa clear anajitahidi na huwa anamwambia, mie sikupendi na wala sitaki tuwe wapenzi pindi anapoona huyu kaka anavuka mipaka na hili husababisha huyu kaka kuchanganyikiwa zaidi, kulia, kubembeleza nk mambo ambayo ni ya hatari zaidi!!
 

lol

Sikujua kama kuna kadhia kama hii ktk karne hii. Kweli hii ni Obsession!
 
Duh amwambia mumewe kabla kitumbua hakijaingia mchanga, kutosema ukweli mapema ni aina ya uongo nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…