Msaada: Ili uchaguzi wa Kenya urudiwe, inatakiwa wagombea wapishane kwa asilimia ngapi kila mmoja?

Msaada: Ili uchaguzi wa Kenya urudiwe, inatakiwa wagombea wapishane kwa asilimia ngapi kila mmoja?

zamlock

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Posts
3,840
Reaction score
659
Wana jf,

Nisaidie kufahamu ili uchaguzi urudiwe kila mtu anatakiwa kuwa na asilimia ngapi ya kura? Kwa sababu mpaka saizi naona wanacheza kwenye asilimia hamsini.
 
Mshindi anapaswa kuwa na 50%+ ya kura zote. Ikiwa mmoja amepata 50% na mwingine 49% au 50%/50% basi uchaguzi utarudiwa. Ama huyo mshindi akiwa hajatimiza 50% pia uchaguzi utarudiwa.
 
ja,an wana jf nisaidie
kufahamu ili uchaguzi urudiwe kila mtu anatakiwa kuwa na asilimia ngapi
ya kura? Kwa sababu mpaka saizi naona wanacheza kwenye asilimia
hamsini

"Hivi Gongolambali na Mboto, wapi mbali?" Kuwa makini na heading zako!
 
Kweli kabisa inabidi mshindi apate 50%+ ya kura zote hapo uchaguzi utakuwa haurudiwi ila akipatikana mmoja akapata 50% au pungufu ya hizo ina maana hajatimiza masharti ya kutangazwa mshindi
 
Asilimia 50 ongeza kura moja .ie. 50%+1 vote only.
 
Msaada please ikiwa Raila akimpita Odinga kwa 50% + 1 mambo itakuwaje.Just joking kichwa cha habari kimekaa mkao wa kuchekesha na mimi nimeamua kuweka habari ya kuchekesha kidogo jupunguza stress.
 
Msaada please ikiwa Raila akimpita Odinga kwa 50% + 1 mambo itakuwaje.Just joking kichwa cha habari kimekaa mkao wa kuchekesha na mimi nimeamua kuweka habari ya kuchekesha kidogo jupunguza stress.

Ha ha ha ha ha ha kwel ww mkali sana
 
Naona watu wengi wanaijua requirement ya at least 50% rule. lakini kuna ile ingine ya at least 25% in at least 24 counties
 
Back
Top Bottom