Msaada: Injini ya gari yangu aina ya Subaru Legacy inatafuna turbo!

Rasputin

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2018
Posts
557
Reaction score
685
Habari wakuu,

Nina Subaru legacy ambayo matatizo yake yalianza mara baada ya kubadilisha timing belt, baada ya hapo cylinder head ikaliwa, baada ya kubadilisha nayo tu baada ya masaa machache turbo nayo ikakata shaft, nikanunua turbo nyingine, nayo pia ikakata shaft, (nahisi shida ni fundi pia maana huku nilipo hizi gari sio common).

Nimepoteza hela nyingi kubadilisha hivyo vifaa na bado gari haitembei, mpaka nawaza nikaikate au niilengeshe kwa mtu.

Mwenye kufahamu shida nini naomba anisaidie, asante!
 
Tumia gharama upeleke miji yenye mafundi. Na kwa kuanzia unaweza peleka DSM,Arusha, Mwanza na hata mikoa ya jirani kama Dodoma au Pwani
 
Upo mkoa gani? ulikuiwa unaagiza spea wapi? kama upo Dar ipeleke kwa God pale kinondoni biafra 0_06
 
Pole Mkuuu.
Utakuta humu Uzi watu wanaponda tunaotumia TOYOTA huku Mikoani, miongoni mwa vitu tunaepuka ni kama hicho unachoalalamikia wewe. Leo gari yako ingekuwa RAV 4 au the like ungekuwa unapeta tu. Anyway jaribu ushauri hapo juu upambane mpaka kieleweke.
 
Hapo kwenya kuilengesha kwa mtu wakati ukifahamu fika ina matatizo ndio nimekuona we hufai hata kupewa mawazonya kusaidiwa.

Kwanni watu mnakuwa na roho za kinyama na kichawi hivi?
 
Hapo kwenya kuilengesha kwa mtu wakati ukifahamu fika ina matatizo ndio nimekuona we hufai hata kupewa mawazonya kusaidiwa.

Kwanni watu mnakuwa na roho za kinyama na kichawi hivi?
Kwanza hata mtu wa kununua Subaru BMW Audi kwa mtu anakuwa hajitambui bora ata hiyo m8 au saba uende showroom uvute vitz yako kiroho safi
 
Mkuu kwani Toyota aiharibiki Mkuu mimi nadhani gari zote zinaharibika ni vile umempata nani sahihi wa kulitengeneza...
 
Hapo kwenya kuilengesha kwa mtu wakati ukifahamu fika ina matatizo ndio nimekuona we hufai hata kupewa mawazonya kusaidiwa.

Kwanni watu mnakuwa na roho za kinyama na kichawi hivi?

Sio kwa maana hiyo, kuilengesha ni mtu ana assess tatizo mwenyewe kama anaona ataweza kutengeneza anaichukua, tena kwa bei ya chini.
 
Utakuwa unanunua spare feki au mafundi hawajui kazi go to the right mechanics
 
Ukisifia Toyota unaonekana mshamba ila kiukweli hizo brand nyengine ni kichefuchefu. Hakuna mtu anayependa gari yake iwe mbovu ila ni asili ya kila kilicho kizima ipo siku kitakuwa kibovu tu.

Sasa je, panapo ubovu uwezekano wa tiba ukoje? Hapo ndipo Toyoda anapoibuka kidedea. Mifumo rahisi ya kuitengeneza na Universal spare parts.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…