Msaada: Ipi ni aina bora ya water pump?

Ze Analyst

Member
Joined
Feb 2, 2019
Posts
49
Reaction score
83
Wadau nipo mbioni kununua water pump kwa ajili ya shughuli za umwagiliaji.

Naomba kujuzwa ipi ni aina bora ya water pump, hasa hizi za inchi 3-4 zinazotumia petrol.

Ahsanteni!
 
Tujuzwe na bei zake pia ziuzwapo.
 
Kwanza inategemea unataka kumwagilia kwa njia ya matone au kwa kutumia sprinkles. kama kwa matone pump ya petrol inatosha lkn kama ni kwa sprinklers basi tumia pump za diesel.

Water pump nzuri ni zile zinazotumia Diesel, utapata unafuu wa gharama za mafuta. Pump za petrol zinauzwa bei ndogo laki 2 mpaka 3.5 lakini zinatumia mafuta mengi.

Na pampu za disel M1 na zaidi zinatumia mafuta kidogo nakushauri nunua pump ya diesel kama uwezo wako utaruhusu.
 
Vipi umezingatia gharama za matengenezo ya water pump ya dizeli(diesel)?
Ninahofia bei ya vipuri(spare parts) na upatikanaji wake hivyo vipuri.

Umezingatia urahisi wa kupata fundi wa hizo pump za diesel huko mashambani kama vijijini?
 
Natumia Bison ya inch 3, Tsh 350,000. Inatosha kabisa.
 
Nenda na pump ya Boss 7HP na inch 3. Bei kama laki 3 bila mpira wala koromeo. Inatumia Petrol.
 
Tafuta pump za Boss ila iwe original imepigwa chapa/ nembo ya chuma maandishi yake kwenye Engen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…