Msaada: Jaji kahongwa

Msaada: Jaji kahongwa

Jamani kweli nimekwama naomba msaada, Niko Mbeya na nina kesi nafuatilia ya mahakama ya Mbeya, nimeshtakiwa kwa kesi isiyo na kichwa wala miguu haina uthibitisho hata mmoja wala shahidi ila nimepelekwa mahakamni na kila siku nakuja kusikiliza kesi. Nimeajiri mwanasheria na ni gharama mnoo hivi Tanzania mtu yeyote anawez kuamua kukupeleka mahakamani bila uthibitisho wowote ni maneno tu na akakusumbua hata miaka mitano kwenda na kurudi mahakamani bila sababu? Na jaji amegoma kufuta kesi wakati mshtaki muda mwingine hatokei yani ni pulkushani tu. Wapi naweza kumshtaki jaji achunguzwe au kubadilishwa jaji maana naona kesi yangu haina kichwa wala miguu ila nasumbuliwa sana
Kazi ya mahakama ni kutoa haki....kwa nn unasema krsi haina kichwa wala miguu? Jaji ataamua tu kwa haki muamini
 
Jamani kweli nimekwama naomba msaada, Niko Mbeya na nina kesi nafuatilia ya mahakama ya Mbeya, nimeshtakiwa kwa kesi isiyo na kichwa wala miguu haina uthibitisho hata mmoja wala shahidi ila nimepelekwa mahakamni na kila siku nakuja kusikiliza kesi. Nimeajiri mwanasheria na ni gharama mnoo hivi Tanzania mtu yeyote anawez kuamua kukupeleka mahakamani bila uthibitisho wowote ni maneno tu na akakusumbua hata miaka mitano kwenda na kurudi mahakamani bila sababu? Na jaji amegoma kufuta kesi wakati mshtaki muda mwingine hatokei yani ni pulkushani tu. Wapi naweza kumshtaki jaji achunguzwe au kubadilishwa jaji maana naona kesi yangu haina kichwa wala miguu ila nasumbuliwa sana
JAJI KAHONGWA NA NANI?
 
sababu

alienishtaki ni kama kanionea yani nimevunja uhusiano wetu wa biashara kisheria kabisa ila sasa kunikomoa kaenda mahamkamni kudai nilimtusi. shida hana ushahidi wowote ila ndo kesi miaka mitano. ni haki kweli?
Kesi ya matusi tokea lini ikaamuliwa na Jaji?Ukiwa muongo at least uwe na kumbukumbu nzuri.
Hii ni chai tu.
 
Jamani kweli nimekwama naomba msaada. Niko Mbeya na nina kesi nafuatilia ya mahakama ya Mbeya, nimeshtakiwa kwa kesi isiyo na kichwa wala miguu haina uthibitisho hata mmoja wala shahidi ila nimepelekwa mahakamnani na kila siku nakuja kusikiliza kesi.

Nimeajiri mwanasheria na ni gharama mnoo hivi Tanzania mtu yeyote anaweza kuamua kukupeleka mahakamani bila uthibitisho wowote ni maneno tu na akakusumbua hata miaka mitano kwenda na kurudi mahakamani bila sababu?

Na jaji amegoma kufuta kesi wakati mshtaki muda mwingine hatokei yani ni pulkushani tu. Wapi naweza kumshtaki jaji achunguzwe au kubadilishwa jaji maana naona kesi yangu haina kichwa wala miguu ila nasumbuliwa sana.
soma hii kesi , mkatae jai
 
Attachments

sababu

alienishtaki ni kama kanionea yani nimevunja uhusiano wetu wa biashara kisheria kabisa ila sasa kunikomoa kaenda mahamkamni kudai nilimtusi. shida hana ushahidi wowote ila ndo kesi miaka mitano. ni haki kweli?
Kuna mahali mwanasheria wako anazembea ama kwa kutojua vizuri kazi yake ama kwa makusudi ili aendelee kupata legal fees na attendance.

Zungumza na wakili wako akupe legal opinion nini cha kufanya, maana kusubiri tu kesi ikitajwa daily sio jambo la kisheria. Unakua kama huna mwanasheria.
 
sababu

alienishtaki ni kama kanionea yani nimevunja uhusiano wetu wa biashara kisheria kabisa ila sasa kunikomoa kaenda mahamkamni kudai nilimtusi. shida hana ushahidi wowote ila ndo kesi miaka mitano. ni haki kweli?
Judge na kesi za matusi wapi na wapi!? Kesi za kutusi nazisikiaga sana huko Mahakama za Mwanzo, na huko hakuna ma Judge!!
 
Shukrani mkuu umenisaidia sana. Kweli JF ni great thinkers.
SOMA NA HII
Kwa hiyo suala sio kuwa Msajili ni mtu kwa kiasi kikubwa anaonekana atapendelea upande fulani, bali suala ni kuwa je mtu wa kawaida anaweza kumtilia shaka juu ya uamuzi wake?

Hivyo ndivyo ilivyoamuliwa na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania katika kesi ya Zabroni Pangamaleza Vrs Joakim Kiwaraka: Civil Appeal No.33/1987. katika kesi hiyo hakimu alingangania kusikiliza kesi wakati mmoja wa wadaawa alimkataa asisikilize kesi hiyo. Jaji Mfalila alisema hukumu hiyo ilikuwa batili, kwani kitu muhimu sio kuwa tu haki inatendeka bali haki ionekane kutendeka wazi kwa mtu wa kawaida. Na akasema kuwa suala sio kulikuwa na uwezekano wa mkubwa wa hakimu huyo kupendelea upande fulani, bali suala ni kuwa je mtu wa kawaida (kama yule mdai aliyemkataa hakimu) angeweza kumtilia shaka hakimu angalau shaka kidogo tu juu ya uamuzi wake? Kesi zingine za Tanzania zinazosisitiza suala hilo ni Mbuji Vrs R.1971) H.C.D. n. 200; R.Vrs Abdallah Msumi: (1973) L.R.T. n.45; Michael Marogwa Leonard Vrs R.:133.

Kuna kesi zingine za nchi za nje zinazosisitiza sual hilo kuwa muamuzi asiwe mtu wa kutiliwa shaka nazi ni:
Metropolitani Properties Co.Ltd. Vrs. Lennon196 3 All E.R. 304 (Uingereza); Livesey Vrs. New Southern Wales Bar Association1985) L.R.C (Const.)580 (Trinidad and Tobago); Law Society of Lesotho Vrs. The Prime Minister: (1986) L.R.C. (Const)508(Dominica).

Utaratibu huo wa kumkataza muamuzi anayetiliwa shaka asishiriki kutoa uamuzi, hauhusu mahakimu pekee bali unahusu hata waamuzi wowote wa vyombo vingine vya dola vingine-tazama hukumu ya Uingereza ya Allinson Vrs. General Council of Medical Education and Registration1891-4)All E.R. Rep. 768.
 
Ni kesi gani hiyo nikupe advocate wa uhakika
Si amesema kuwa tayari ana mwanasheria? Au mwanasheria wake unamfahamu kuwa sio wa uhakika?

In short, aliyekushtaki ndiye shahidi namba moja. Na shahidi mmoja tu anatosha kuithibitishia mahakama na ikafikia uamuzi. Kuhusu kesi kuchukua miaka mitano, mbona mingi sana? Na siku hizi mahakama inakataza backlogs za kesi. Ila unaweza kuiomba mahakama ikasikiliza upande mmoja.

Kama una ushahidi wa hongo aliyopewa Jaji, basi nenda TAKUKURU. Ama lah, iombe mahakama ikubadilishie Jaji. Onesha kuwa huna imani nae kwa kuwa amehongwa "ushahidi uwepo" sio blah blah tu za vijiwe vya kahawa.

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
 
Jamani kweli nimekwama naomba msaada. Niko Mbeya na nina kesi nafuatilia ya mahakama ya Mbeya, nimeshtakiwa kwa kesi isiyo na kichwa wala miguu haina uthibitisho hata mmoja wala shahidi ila nimepelekwa mahakamnani na kila siku nakuja kusikiliza kesi.

Nimeajiri mwanasheria na ni gharama mnoo hivi Tanzania mtu yeyote anaweza kuamua kukupeleka mahakamani bila uthibitisho wowote ni maneno tu na akakusumbua hata miaka mitano kwenda na kurudi mahakamani bila sababu?

Na jaji amegoma kufuta kesi wakati mshtaki muda mwingine hatokei yani ni pulkushani tu. Wapi naweza kumshtaki jaji achunguzwe au kubadilishwa jaji maana naona kesi yangu haina kichwa wala miguu ila nasumbuliwa sana.
Ndugu ikiwa umemwajiri mwanasheria (wakili) ili kukuwakilisha mahakamani katika kesi inayokukabili basi unapaswa kuamini katika uwezo wake.

niwazi kuwa ulijiridhisha juu ya uwezowake kabla mpaka ukaamua kumpa kazi.

NB: Hii imekuwa tabia ya wateja wengi Tanzania kutafuta au kutoamini mtaalamu wa Sheria anachokishauri. Nikuombe utulie na wakili wako HAKI kama ipo ipo tu inakuja.
 
Ni vema
Ujue kwamba nia yangu sio kutoamini mwansheria bali kutoamini mahakama. Nadhani mnafahamu fika kwamba mahakama nyingi hazina haki. Usipindishe maana yangu tafadhali. Hata mwanasheria wangu naona anapata shida na kupotezewa muda ilhali anafuata kanuni vema kabisa. Anaweka vikwazo wanamzungusha. Sasa hapo ana shida gani? Hana shida. Enenda na ushauri wako hauna maana kabisa kwa hio context
 
Back
Top Bottom