Msaada Jamani kuhusu metabolic rate watu wembamba na wanene, ninaangukia wapi?

Tangopori

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2012
Posts
1,628
Reaction score
1,285
Habari zenu wakuu!

Mimi ni kijana wa miaka 24 kuna mabadiliko yalitokea katika maisha yangu japo sio makubwa saana ila yamenifanya nijiulize maswali mengi ya kibiolojia sasa naomba madaktari na wale wenye ufahamu wanisaidie!
Kitu chenyewe ni kwamba mimi nilivyokuwa mdogo hadi nilivyomaliza form four nilikuwa mwembamba sana na nakumbuka nilikuwa nakula chakula kingi sana siku nyingine hata asubuhi nilikuwa nakula kiporo kingi kama chakula cha mchana(nimekulia kijijini) na pia sikuwa mtu wa mazoezi nilikuwa na na maisha ya kawaida!
Ila nilivyomaliza form four nikaanza kupata afya, ikaendelea kupanda tu taratibu taratibu baada ya muda kila nikikutana na mtu ananiambia aisee umenenepa(kulingana na jinsi nilivyokuwa mwanzo) japo nilikuwa nakula the same na nilivyokuwa nakula mwanzoni hadi sasa hivi kuna kakitambi kananinyemelea!
Sasa wakuu siipendi hali hii na kibiolojia najua kuwa mwanzoni inawezekana metabolic rate yangu ilikuwa high na sasa hivi inawezekana iko low!
Je hii inaweza ikasababishwa na nini?(maana hata kula nimepunguza)
Kiukweli nilikuwa naipenda sana hali yangu ya mwanzo kuliko hii niliyonayo sasa!
Kinachoniwazisha sana ni haya mabadiliko yaliyotokea na namna yalivyotokea nikiangalia nyumbani kwetu wadogo zangu wote ni wembamba, mzee mwembamba mama mwembamba!
I really miss my body of that time nikijiangalia kwenye picha natamani niwe na umbo lilelile!
Cc. MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…