Msaada jamani:Mke wangu ana mimba lkn ameona dalili ya hedhi.

Msaada jamani:Mke wangu ana mimba lkn ameona dalili ya hedhi.

Jasho la Damu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Posts
956
Reaction score
120
Naomba msaada jamani mke wangu ana mimba ya miezi miwili na wiki moja ambayo ndiyo mara ya kwanza kushika mimba lkn leo ameona dalili ya hedhi kutoka baada chupi yake kuonesha ina damu kidogo lkn damu hiyo haijaendelea tena na wala hasikii maumivu yoyote katika tumbo lake hii ni dalili ya nini jamani?
 
Hello Brother, why dont you just take her to the Hospital? waweza pata ushauri hapa mzuri tu na tuna wataalam safi sana hapa Jamvini, however kuna cases nyingine ambazo daktari labda atahitaji aonane na Mgojwa direct ili aweze ku analyse and individual case?! when it comes to my wife and a baby, I cant sleep with unresolved issues, go to the Hospital Brother!

Naomba msaada jamani mke wangu ana mimba ya miezi miwili na wiki moja ambayo ndiyo mara ya kwanza kushika mimba lkn leo ameona dalili ya hedhi kutoka baada chupi yake kuonesha ina damu kidogo lkn damu hiyo haijaendelea tena na wala hasikii maumivu yoyote katika tumbo lake hii ni dalili ya nini jamani?
 
Mie nakushauri nenda hospitali esp kama ni damu imetoka ili waangalie na nyie mtulie kutofikiria sana ili au lile.

naomba hii isikutishe ila mara nyingi kutoka damu sio kitu kizuri huwa inaashiria kupoteza mimba,na pia inaweza kuwa ni damu ya zamani iliyoko kwenye ukuta humo ndio imetoka hii aina madhara kwa mimba.

Kama alivyosema mdau hapo juu, hata mie nisingelala na hilo. kimbilia hopsitali yenye daktari wa mambo ya mimba. kwa sasa lazima kama kuna uhai wa mtoto utaonekana I mean heartbeat. wakim scan wataona yoyte yanayoendelea kwenye womb.

Good luck.
 
wakuu nashukuru kwa ushauri wenu nitaenda kesho hospital ya wilaya maana huku nilipo ni kijijini ikifika saa 12 kumpata dr.ni shughuli.
 
...Inawezekana hakuna tatizo lolote na ujauzito wake lakini ili kupata uhakika inabidi kuwahi hospitalini ili Wataalam wakamuangalie vizuri na kuhakikisha kila kitu kiko salama.
 
Napenda kuwapa matokeo ya ushauri wenu: leo nimempeleka mke wangu hospital kama mlivyonishauri amechekiwa kwa Ultrasound na imegundulika mimba ina miezi mitatu na wiki moja na si miezi 2 kama nilivyosema awali pia mtoto anaendelea vizuri hana tatizo lolote.
Nawashakuru sana wanaJF Godbless u ol.
 
Hali hiyo huwa inatokea kwa wajawazito mara moja moja, ila mpeleke hospitali haraka.

Kwa kuwa ni mimba yake ya kwanza, unapoona kitu chochote kinachokuletea mshangao mpeleke harak hospitali au kama ana daktari wake basi uwe unampigia simu wakati mwingine anaweza kukushauri ufanye nini au anywe dawa gani, lakini usisubiri kushauriwa na watu, maana madaktari wa mtaani wako wengi watakushauri mpaka utachanganyikiwa, we muone daktari kwa ushauri sahihi
 
hilo linatokea hasa kwa mimba inapokuwa ndogo..... ingekuwa mimba ni kubwa basi ingekuwa ni shida,,, hata my waifu wangu ishatokea hilo.......
 
apime na group ya damu, kama yeye yuko labda b negative nawewe O positive ajiandae kuchoma sindano ya ant D mtoto atakapozaliwa akiwa na damu tofauti na group lake, pili acheki placenta kama iko chini sana au la, hii inaitwa low lying placenta (placenta previa) nayo inasababisha damu kutoka bila maumivu japo maranyingi inakua kwa mimba ya miezi 6 na kuenelea, Pia aepuke kuinama inama, kunyanyua uitu vizito, stress nk. KILA LA KHERI
 
wahi hospital wana weza kutatua tatizo
 
nenda hospitali mwone daktari piaufanyiwe na vipimo, hutokea bmara chache lakini huwa sio nzuri,
hadi ina[pothibitishwa mimba ipo salama.
 
Nenda hospital, hilo lilishamtokea mpenzi wangu, tukaenda hospital tukaambiwa mimba imetunga nje ya kizaz ni hatari sana tukashauriwa asafishe kizazi.
 
Naomba msaada jamani mke wangu ana mimba ya miezi miwili na wiki moja ambayo ndiyo mara ya kwanza kushika mimba lkn leo ameona dalili ya hedhi kutoka baada chupi yake kuonesha ina damu kidogo lkn damu hiyo haijaendelea tena na wala hasikii maumivu yoyote katika tumbo lake hii ni dalili ya nini jamani?
Mimba imetungwa nje ya mfuko wa kizazi. Hii inatokana na mwanamke kuwa hodari wa kuchoropoa sana mimba
 
Napenda kuwapa matokeo ya ushauri wenu: leo nimempeleka mke wangu hospital kama mlivyonishauri amechekiwa kwa Ultrasound na imegundulika mimba ina miezi mitatu na wiki moja na si miezi 2 kama nilivyosema awali pia mtoto anaendelea vizuri hana tatizo lolote.
Nawashakuru sana wanaJF Godbless u ol.
Bila shaka huyu mtoto sasa huvi yupo darasa la pili na ana mdogo ake wakucheza nae!!
 
Back
Top Bottom