Msaada jamani njia za kienyeji za kutunza vifaranga vya kuku wa kienyeji wangu wanakufa sana!

Msaada jamani njia za kienyeji za kutunza vifaranga vya kuku wa kienyeji wangu wanakufa sana!

ufumawicha

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
504
Reaction score
209
Wana JF niokoeni mwenzenu, niko Mpanda ambako chanjo za kuku hazipatikani sana. Nishaurini njia rahisi za kienyeji za kulea vifaranga kwani huo ni mtihani ambao umenishinda nami nataka kuwa na kuku hadi 1000 kwani kwa sasa nina jogoo 3 na jike 12. TATIZO KULEA VIFARANGA HADI VIKUE NDIYO MTIHANI HATA INGAWA NINA BANDA.
 
kuna uzi humu sticky unaelezea kila kitu jukwaa la ujasiriamali acha uvivu!
 
Hivi kwa wastani hekari moja inatoka kiasi gani, na gharama za kuhudumia shamba kuanzia mwanzo mpaka mavuno zikoje kwa anayefahamu.
 
mtafute Mama Joe atakusaidia kwa hilo!
 
Last edited by a moderator:
mtafute Mama Joe atakusaidia kwa hilo!
duh! Mimi huwapa chanjo lakini kienyeji pure shambani mlinzi amekataa nisiwape anawatwangia aloe vera mara kwa mara anawapa kwenye maji yao. Dawa zingine majani ya mlonge wanakula na maji yake kuchemshwa na kunywewa. Mipapai mbegu hutiba macho yenye uvimbe usio ndui. Mafuta alizeti hupakwa uvimbe wa ndui. Kwenye uzi zijue mbinu zangu.... Wa Kubota niliweka pdf document inaelezea hizi dawa ufungue. Pia juzi kuna mtu kaelezea aloe vera na manjano. Karibu mkuu.
 
Last edited by a moderator:
wana jf niokoeni mwenzenu,niko mpanda ambako chanjo za kuku hazipatikani sana.Nishaurini njia rahisi za kienyeji za kulea vifaranga kwani huo ni mtihani ambao umenishinda nami nataka kuwa na kuku hadi 1000 kwani kwa sasa nina jogoo 3 na jike 12.TATIZO KULEA VIFARANGA HADI VIKUE NDIYO MTIHANI HATA INGAWA NINA BANDA

Utunzaji wa Vifaranga wa Kuku wa Kienyeji ni mgumu sana, kwa sbabau ya nature yao ni kama ilivyo kutunza vifaranga vya kware, ninishu, Kufa kuna sababishwa na mambo mengi sana kama vile.#
1. Baridi- Hili ndo kubwa sana linalo waua vifaranga.
2. Magonjwa kama COCCIODIOSIS-
3. Typhoid nk

Kukosekana kwa chanjo hakuwezi kukawa chanzo cha vifaranga kufa kwa sababu ugonjwa kama kideri hujitokeza baadae na kuna kuku ambao hawajawahi chanjwa kabisa, ingawa ni muhimu sana kuwachanja. Ila zingatia maswala ya Baridi.
 
wana jf niokoeni mwenzenu,niko mpanda ambako chanjo za kuku hazipatikani sana.Nishaurini njia rahisi za kienyeji za kulea vifaranga kwani huo ni mtihani ambao umenishinda nami nataka kuwa na kuku hadi 1000 kwani kwa sasa nina jogoo 3 na jike 12.TATIZO KULEA VIFARANGA HADI VIKUE NDIYO MTIHANI HATA INGAWA NINA BANDA

Ukitaka watu washauri na waweze kukusaidia lazma ueleze kwa mapana na kwa ufasaha,mf hukueleza vifaranga vinavyokufa hukumbwa na tatizo gani? au wanapoumwa huonesha ishara gani ya tofauti,
mf kinyesi chao kikoje?nk.
Hapo itakua rahisi watu kushauri,
Ila kua makini sana na baridi ika nje ya hapo wanaeleze watu japo ishara flani ya tofauti itakia rahisi kisaidiwa.Vinginevyo utapata kila aina ya maelezo ambayo yanaweza yasilenge tatizo lako
 
Back
Top Bottom