Tatizo la kigugumizi huwaathiri kiasi cha aslimia moja ya watu wazima katika jamii yoyote duniani. Mara nyingi ni tatizo la kurithi. Wanaume wengi huwa na shida hii ukilingainisha na wanawake. Kwa watoto chini ya miaka 5, asilimia 5 huwa na kigugumizi, bahati nzuri kati ya hao wengi kigugumizi hupotea wakati wanapoanza shule ya msingi, na ndio maana idadi hupungua kutoka 5% hadi 1%.
Tiba nyingi zimejaribiwa bahati mbaya hakuna ambayo imeleta mafanikio ya kutosha.
Hata hivyo kuna tabia za wazazi ambazo zimeonesha kuzidisha hali hiyo au kuzuia kabisa isipotee, au kuzuia watoto wenye shida hiyo wasipate nafuu. Tabia hizo ni za ukali na kujaribu ama kuwakosoa wanapoongea au kuwasahihisha.
Kwa hiyo kama mtoto wako ana shida hii usijaribu kumkaripia anapoongea au kumkosoa au kumsahihisha, na unapoona amekosoa jaribu kumweleza polepole. Kama anaongea na anachelewa kumaliza sentence usijaribu kumsaidia kumalizia hiyo sentenci. Ishi naye kama vile hiyo shida haipo na baada ya muda utaona imeisha au imepungua kwa kiasi kikubwa,