msaada jamani


Jerda huyo jamaa hakupendi hata kidogo kwa sababu zifuatazo:

1. Tayari ana mtu mwingine kabla yako, Je unajua ana muda gani na huyo demu mwingine? Je huyo mwingine anajulikana kwao? Kama kweli anakupenda asingekuwa na mwingine au angekutaarifu mapema kabla ya kuanza uhusiano nae.

2. Ni kwanini siku hiyo alikuambia muachane? Na alikutamkia mara 3 kutokana na maelezo yake hapo juu, yaani yaonekana alikuwa ana uhakika wa 100% na alikuwa anasema. Mimi napata picha ya kuwa anampenda yule zaidi yako na ndio maana alikuambia muachane. Alikuwa anataka uhuru zaidi na huyo demu mwingine.

3. Je umejaribu kuchunguza huyo demu wake mwingine yupo wapi ? Naye ni mwanafunzi km wewe au (Yawezekana ni mfanyakazi na ana maisha mazuri sana)? Soma bibie upate elimu yako huyo jamaa atakuchezea tu. Mwishowe utakosa vyote utakuja juta maishani mwako!

4. Mpo kwenye mahusiano mwaka wa tatu sasa, siku zote hizo hukugundua kama ana demu mwingine? Kwa nini basi msioane km kweli anakupenda? Huyo jamaa shida yake ni kukuchezea tu kama angekuwa yupo serious kwako angetangaza ndoa mapema sana?


Napata picha ya kuwa hata wewe mwenyewe bado upo kigeugeu yaani "sitaki nataka"! Kazi ni kwako mwanamke kusuka au kunyoa. Kaa chini tafakari na chukua hatua!
 
duh, nimepata ujasiri ngoja nifanye maamzi magumu
 
Hongera, ila nahisi bado kuna mengi umeficha!
Naomba jibu kwenye namba mbili hapo juu nilipouliza "Kuna tukio gani lililotokea hadi ukajua ya kuwa ana demu mwingine na kusababisha kukutamkia "muachane mara tatu"?"
 
mie nilikutana na situation kama yako tena nikiwa na mtoto wake, mambo yakageuka. Nikafanya maamuzi magumu ya kumtoa moyoni, kwa sasa na enjoy na mwanangu no stress at all.
 
Ukweli ni kwamba hakupendi ,anajua unampenda so siku akikosa wa kugonga ndio anarudi kwako
Kimbia haraka sana na fuata ushauri wa kaka hapo juu wa kubadili number
 
kila kubwa ina kubwa yake....
find it..lol
 
Ukweli ni kwamba hakupendi ,anajua unampenda so siku akikosa wa kugonga ndio anarudi kwako
Kimbia haraka sana na fuata ushauri wa kaka hapo juu wa kubadili number
naweza sema hapana bcoz kila siku asubuhi mchana na jion alikua ananicall, na tulikuwa na mgogoro march alikuja home kila wknd kuomba msamaha na me nikikazia kumtreet kama rafiki, sema mwz wa kumi amesamehewa ndo matatizo yakafuatana kama maji vile, nakumtell kuwa nilikuwa nimempa last chance basi kashindwa ndo vile...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…