Kwa kawaida mahakama pekee ndio ina mamlaka ya kusema ndoa imevunjika na kimsingi mahakama haivunji ndoa ila inatamka (declare) kuwa ndoa imevunjika. Na kuna sababu zilizotajwa na Sheria ya Ndoa zinazoweza kusababisha ndoa ivunjike.
Kwahiyo kama ungesema wewe na mwenzako mna shida gani, tungeweza kukushauri. Hatahivyo suala la mgawanyo wa mali haliangalii kuwa una watoto au hauna, kinachoangaliwa ni mchango wako katika kupata mali mliyokuwa nayo na haijalishi kama wewe ulikuwa unafanya kazi au la kwani katika kesi ya Bi Hawa Mohamed, mahakama ilisema hata mama wa nyumbani anastahili kupata mgao wa mali.