Nimeanza kufanya mazoezi ya kukimbia asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi hua natoka huku town kuelekea mlimani sasa kila siku hua naenda fresh tu bila.tatizo ila sasa nikifika kule juu ambapo ndo mwisho napogeuzia na nikianza kushusha (kurudi) hua napata maumivu upande wakulia maeneo ya tumboni sasa sijui niseme ni kichomi? kwa kweli sijui ni nini na kila nikirudi tu ndo hua hili tatizo linaanza na pia nikiwa navuta pumzi ndani kwa nguvu hua panauma pale (wakati nakua na rudi huku na kimbia). kwa hio ninomba msaada kwa anaejua maana naogopa.sije ikawa ni appendicitis