Pole na changamoto.
Kutokana na maelezo yako ni kuwa sphincter iliyo kati ya esophagus na stomach haifanyi kazi sawasawa.
Hali hiyo inaweza kusababishwa na vitu vingi pamoja na matatizo ya ubongo, infection, hernia ya esophagus, uvimbe tumboni.
Iwapo hali hiyo itaendelea miaka mingi, inaweza kubadili tabia ya ukuta wa esophagus ambao haujazoea kugusana na asidi ya tumboni, jambo linaloweza kusababisha kansa.
Cha kufanya: hali yako inaweza kuwa serious zaidi ya unavyodhani. Ni vema ukaonwa na daktari wa magonjwa ya tumbo (gastroenterologist) ili atathmini ukubwa wa tatizo na kupanga matibabu.
Again, pole na changamoto.