Lakini pia anapokaribia kwenda katika siku zake, mwili hu-sense (huwa unajiimarisha) kukabiliana na kiasi cha damu kitakachopotea katika siku hizo kadhaa, katika kujiandaa huko, mwili utazuia sehemu kubwa ya maji kutotumika kiholela (unayahifadhi kwa dharura inayotegemewa kutokea), si unajuwa maji ni uhai?.
Unajuwa kuwa asilimia 94 ya damu ni MAJI?, ni kama kusema kwa kila lita 10 za damu, lita kama 9 hivi ni maji na lita 1 ndiyo damu yenyewe. Damu huishi ndani ya MAJI, maji yanaweza kuwepo bila damu, ila kamwe damu haiwezi kuwepo bila maji. Hata ukijikata kwa bahati mbaya utaona maji mekundu yakitiririka, sisi huyaita maji hayo kuwa ni damu, ukweli ni kuwa hayo ni maji, damu huwa ndani ya hayo maji na pengine hatuwezi kuiona damu kwa macho pekee bila darubini.
Mwambie ajitahidi kunywa maji, asisubiri kiu ndipo anywe, tena mwambie asinywe maji ya kwenye friji, anywe ya kawaida tu, pengine anaweza kunywa juisi juisi za matunda (juisi aliyotengeneza mwenyewe, siyo ya dukani).
kama atahitaji kweli mtoto ili maumivu (ambayo kwa sehemu kubwa ni ishara za mwili kuwa na usawa mdogo wa maji), mwambie ani-PM naweza nikamsaidia.
Nyumbani | maajabuyamaji.net