Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,768
- 3,622
mimi nimefungua access bank -- mikopo hawanaga longo longo nyingi kama mambenki makubwa. ile ina deal na wajasiriamali wadogo wadogo.
Habari zenu wana JF. Mimi ni mfanyabiashara. Nina kampuni yangu ambayo nimeianzisha hivi karibuni ambayo ninataka kuifungulia account yake. Ninaomba msaada wenu kwa yeyote mwenye ufahamu wa kutosha kuhusu mambo ya mabenki aweze kunishauri benki nzuri inayofaa kwa kufungua account ya biashara au kampuni. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa yeyote ambaye atajitokeza kunisaidia katika hili. Asante
Nakushauri fungua CRDB imekaa kirafiki na mteja, NBC ni ya kibiashara zaidi, NMB soi mbaya sana ingawa ina urasimu wake. Pia ushauri utakaoupata jukwaani hapa hata nawe utaufanyia kazi kwani mpaka unafikia kufungua buz accont ina maana hukuwa unatumia kibubu.
vi upo? Si uliaga kwenda shule,ha ha ha ha ha hapa ndo jf bwana.Ngoja wataalam waje kukushauri
samahani mkuu nadhani umetoka nje ya mada kidogo. Mimi ninahitaji kufungua account kwa ajili ya biashara au kampuni na si vinginevyo
Unapofungua account na hasa kwa ajili ya biashara ni muhimu sana kuangalia benki amabayo iko friendly na ina uwezo wa kukuwezesha kwa njia mbali mbali hasa mikopo ya masharti nafuu ili uweze kukuza biashara yako zaidi. Kwa hiyo mdau aliyekushauri kuhusu Access bank hajakosea kabisa. Kumbuka inaweza ukawa na mtaji leo, kesho mtaji ukapungua au ukapata opportunity nzuri ya biasha ambayo itakuhitaji kuongeza mtaji ili kum meet requirements, kwa hiyo if you are running with good bank they will be there to assist you.
nadhani CRDB ni nzuri; Hii analysis imetokana na mazungumzo nilyokuwa na ma Director wa Business Accounts hapo Tanzania; lakini ni siku za mwanzoni, tunaendelea kuwafahamisha kuhusu nini kinaendelea;
Young_Master,
Mimi ningependa kujua kwanza wewe biashara yako kubwa? ndogo ? au ya kati?
Pili je unategemea kufanya transactions za aina gani? ni TISS transfers Ambayo ni kutuma pesa account ya benki moja kwenda nyingine? au utafanya sana Telegraphic Transfers (swift) nje ya nchi au transactions nyingi ni ku deposit na ku withdraw, au kubadilisha currency tofauti?
Zingatia yafuatayo utakapoenda kuongea na benki (1) Charge ya kila mwezi (2) Charge ya kila transactions (3) Charge ya ku deposit/withdraw pesa kwenye acc yako (4) Kiwango cha kutoa bila notice
Kuna benki ambazo huwezi siku kukurupuka kwenda kuchukua milioni 20 wanataka notice ya siku moja, kama biashara yako ipo spontaneous aisee uta suffer.
Mimi ningeshauri uende kwenye benki ndogo ambazo ni more customer focused and hazina mlolongo na mistari, ukiwa mfanyabiashara hutakiwi ukae benki 1 - 2 hrs. Achana na NMB , CRDB na NBC.
Mkuu nenda FNB kafungue account, service zao ni nzuri
Ni kwa nini nikafungue account FNB badala ya benki nyingine. Unadhani FNB inatoa huduma gani bora ambazo zitanishawishi mimi kama mteja kwenda kufngua account kwao? Na je benki hiyo itaninufaishaje mimi na bishara yangu?