Business Plan sio kitu rahisi cha kuelezana kwenye post kama za humu. Ina contents za kutosha kabisa. Na hata mtu akikupa sample, inabidi uwe na uelewa wa kutosha kuibadili hiyo sample kuwa katika idea yako. Kwa ufupi, kama hukuwahi kufundishwa kabisa uandishi wa Business Plan, ni vyema ufanye moja ya mambo kati ya haya mawili:
1. Tafuta mtu akufundishe uandishi wa Business Plan (naamini itakuchukua kama wiki mbili hivi ili kuajua kwa undani kila kipengere cha Business Plan) AU
2. Tafuta consultant mmoja wa mambo ya biashara mkutane naye, umpe idea yako, akae nayo walau wiki moja, then aje akupe Business Plan
NB: Business Plan inatoa mwelekeo wa idea ya biashara unayoitarajia kufanya. kwa mantiki hiyo, jibu la muelekeo linaweza kuwa UENDELEE au USIENDELEE na wazo la hiyo biashara, kwamba itakulipa au haitakulipa. Kwa mantiki hiyo, nakushauri ujifunze mwenyewe namna ya kuandaa B/P ili uingie gharama mara moja tu yaani gharama za mafunzo. Ukipeleka kwa consultant, huenda ukalazimika kumlipa kila unapopeleka wazo jipya baada ya wazo la awali kutoonyesha matumaini. Kama ukiwa na elimu mwenyewe, utajaribu mawazo yako kadhaa bila ya kikomo na bila ya gharama za ziada.