Msaada jinsi ya kuanzisha limited company...

sexologist

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
2,276
Reaction score
976
Wanajamvi poleni kwa majukumu..

Mimi ni mtanzania ambaye nina nia ya dhati kuanzisha kampuni itakayokuwa inajihusisha na maswala ya kilimo.. Tafadhari naomba nisaidiwe taratibu na namna ya kuanzisha kampuni hiyo.. na pia nisaidiwe kufahamishwa kama kuna gharama zozote zinahitajika mwanzoni au kama kuna malipo ya aina yeyote.

Mawazo yenu waungwana ninayaheshimu sana.
Natanguliza shukrani zangu za dhati.


Ni mimi
mbumbumbu mwenye akili
 
Mr Mbumbumbu ujambo?
Tayari una dira na mwelekeo wa shughuli za kampuni yako tarajiwa "Kilimo". Nikupongeze kwa wazo lako zuri. Mchakato wa kuanzisha Kampuni umekwisha uanza na lazima umekwishaamua na kampuni yako itakuwa na mtaji kiasi gani. Kinachofuata ni kubuni majina unayoyapendelea kampuni yako iitwe na kuyapeleka Brela ili kupata Name Clearance. Hatua itakayofuata ni kuandaa Memorandum and Articles of Association. Kwa uhakika hili unaweza kumtask Lawyer na gharama zake ni kidogo tu (affordable). Kimsingi name clearance & prep of memorandum and articles vyaweza kufanywa sambamba. Hatua itakayofuata ni kufanya usajili brela ambapo gharama za usajili zitategemea kiasi cha mtaji unaotajwa kwenye Memorundum and Articles of Association. Kwa ushauri zaidi ni PM.
 
Kaka kama utahtaj msaada zaidi mtafute huyu mtu nina iman atakusaidia.Ni mtu muaminifu atakusaidia kufatilia kila kitu had kampuni yako kusajiliwa.0714074040
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…