Kaeni kikao cha ukoo wa familia na mteue msimamizi wa Marathi, mkisha mteua anapashwa kwenda mahakamani kufungua shauri la mirathi kuthibitishwa na nyaraka anazopaswa kwenda nazo mahakamani ni Muhtasari wa kikao na cheti cha kifo cha marehemu. Baada ya Mahakama kumthibitisha msimamizi wa mirathi atajaza fomu ambazo zitamtambulisha na atakukuwa na nguvu ya kisheria kushughulika na mali zote alizoacha marehemu ikiwa ni pamoja na kufuatilia stahili zake alizoziacha marehemu kazini, pesa benk, kukusanya na kulipa madeni na kugawa mali hizo kwa warithi halali wa marehemu.