Msaada jinsi ya kuimport tractors kutoka UK

Cvez

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2018
Posts
4,405
Reaction score
13,411
Habari Wakuu!

Husika na kichwa cha habari hapo juu nahitaji msaada kwa mwenye uzoefu au details za jinsi ya kuimport tractor (s) kutoka UK kuja Tanzania.
 
Nimekaa siti ya mbele kabisa kusubiri majibu ya wazoefu wa suala hili! Hakika yatanisaidia sana na mimi.
 
Ninachofahamu ni kwamba zana za kilimo hazina ushuru, kwahiyo likishafika bandarini utalipia tu gharama za pale bandarini za kutoa mzigo wako. Pia unaweza watumia mawakala wa clearing and forwarding (si gharama kubwa ni maelewano tu)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka kununua kabisa huko huko ? Kuna mdaua anaitwa Chris Lukosi mcheki FB uangalie na mizigo kabisa, biashara legit .
 
Unataka kununua kabisa huko huko ? Kuna mdaua anaitwa Chris Lukosi mcheki FB uangalie na mizigo kabisa, biashara legit .
Asante Mkuu nitamcheki naweza pata ABC ingawa issue yangu ilikua importation tu.
 
Howard and sons hawa nawajua vizuri nilifanya nao biashara na kuwapa idea mda mrefu sana uliopita
Wajaribu hao


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Usilaghaikee na wasemao kwa tractor halina malipo forodhani.Utalipia yafuatayo. Kama gharama CIF ni X

1. Wharfage charges 1.85%
2. Port handling charges 2.2%
3. Corridor levy 0.09%
4. VAT 0.41%
5. Shipping line charges 5%
6. Railway Development Levy 1.5%
7. Custom processing fees 0.6%
8. Registration fees Tsh 20,000
9. Number plate fees Tsh 32,000
10. Agency clearing and forward fee (makubaliano yenu)

Weka tayari na takriban dola 100 ya rushwa. Maaana mzigo wako utakawizwa kutoka kwa makusudi mpaka siku ya mwisho ya grace period. Kisha watakwambia Mzigo hauwezi toka leo, na usipotoka leo, kwanzia kesho utatozwa storage fees, ambayp ni dola kadhaa kwa siku. (takriban dola 30 kama nakumbuka vizuri).

Kisha watakwambia, ukazungumza nao vizuri, mzigo waweza upata usiku wa siku hiyo ya mwisho, kabla ya kesho yake. Hapo uandae rushwa ili upate mzigo wako kwa grace period kwisha.
 
Asante sana kwa maelezo yanayojitosheleza. Ubarikiwe ndugu!!!
 
kama haya yana ukweli; ziara ya kushitukiza inatakiwa tena. tumalizie kama tulivyoanza.

inaonekana watendaji waliokunywa uji wa rushwa ni vigumu mno kuusahau utamu wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gharama za port charge zinategemea na CBM ya mzigo. Pia kodi inategemea na gharama za ununuzi.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…