britanicca
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 16,295
- 33,994
Wakuu mi nataka kujua ni aina gan ya bidhaa naweza kuingiza toka dubai kama nina milion nane je nauli na gharama za kwenda na kurudi zikoje
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nashukuru mkuu kiogwe nilipotea kidogo lakini sasa nipo hewani,bwana britanicca wazo lako ni zuri.Pesa yetu inashuka thamani kwa kasi ya ajabu hiyo 8ml ni sawa kama na US $ 3900 na kwa pesa ya hapa Dubai ni kama UAE dhs 14200.Hoteli ya chini kwa sasa ni $75 na ndege ya chini ni Fly Dubai return ticket ni $400 (keep on changing ).Kwa kiasi hicho cha pesa nakushauri mambo mawili,kwanza kwa kuwa ni safari yako ya kwanza Dubai(sina uhakika)basi ifanye mwezi ujao wakati wa Ramadhani kipindi hicho ndege zinakuwa chini,hoteli zinakuwa chini na maduka mengi yanakuwa na mapunguzo ya bei.Kwa sasa hiyo pesa itatosha vizuri kununua mzigo ambao hauutumi (Shipping)ili kuepuka usumbufu wa usafirishaji na bandari bali wawezanunua vitu vidogovidogo ambavyo si vizito sana kama vifaa vya simu pamoja na simu chache au comptuter ambavyo waweza weka kwenye begi na kurudi navyo,zaidi wawezapata idea ya gharama ya vitu kwa kuangalia souq.com au awok.com japo wewe utapata kwa chini zaidi kwakuwa unachukua mzigo mkubwa.Nadhani nimekupa picha japo sijui wewe unapendelea kununua nini.
Samahani mkuu mimi nataka kuanzisha biashara ya jewwlls(heleni,cheni,mikufu,vidani) Je gharama ya kuvitoa Dubai au china ikoje? Na jee quality ya vito vya Dubai zinalingana na vito vya china?
Samahani saana naomba msaada wako maana mie nina kiasi cha pesa kama hicho ila mimi nataka niagize na sio kufata mwenyewe huko DBI
lucky kama unashauri mtu unadhani mtaji wa kawaida sana wa kuanzia kuchukua bishara dubai unaweza kuwa kiasi gani na biashara zipi ambazo zinaweza kumlipa kwa haraka?
Uko vizuri mkuuNashukuru mkuu kiogwe nilipotea kidogo lakini sasa nipo hewani,bwana britanicca wazo lako ni zuri.Pesa yetu inashuka thamani kwa kasi ya ajabu hiyo 8ml ni sawa kama na US $ 3900 na kwa pesa ya hapa Dubai ni kama UAE dhs 14200.Hoteli ya chini kwa sasa ni $75 na ndege ya chini ni Fly Dubai return ticket ni $400 (keep on changing ).Kwa kiasi hicho cha pesa nakushauri mambo mawili,kwanza kwa kuwa ni safari yako ya kwanza Dubai(sina uhakika)basi ifanye mwezi ujao wakati wa Ramadhani kipindi hicho ndege zinakuwa chini,hoteli zinakuwa chini na maduka mengi yanakuwa na mapunguzo ya bei.Kwa sasa hiyo pesa itatosha vizuri kununua mzigo ambao hauutumi (Shipping)ili kuepuka usumbufu wa usafirishaji na bandari bali wawezanunua vitu vidogovidogo ambavyo si vizito sana kama vifaa vya simu pamoja na simu chache au comptuter ambavyo waweza weka kwenye begi na kurudi navyo,zaidi wawezapata idea ya gharama ya vitu kwa kuangalia souq.com au awok.com japo wewe utapata kwa chini zaidi kwakuwa unachukua mzigo mkubwa.Nadhani nimekupa picha japo sijui wewe unapendelea kununua nini.