Msaada jinsi ya kuingiza bidhaa toka Dubai na gharama zake

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Wakuu mi nataka kujua ni aina gan ya bidhaa naweza kuingiza toka dubai kama nina milion nane je nauli na gharama za kwenda na kurudi zikoje
 
Nashukuru mkuu kiogwe nilipotea kidogo lakini sasa nipo hewani,bwana britanicca wazo lako ni zuri.Pesa yetu inashuka thamani kwa kasi ya ajabu hiyo 8ml ni sawa kama na US $ 3900 na kwa pesa ya hapa Dubai ni kama UAE dhs 14200.Hoteli ya chini kwa sasa ni $75 na ndege ya chini ni Fly Dubai return ticket ni $400 (keep on changing ).Kwa kiasi hicho cha pesa nakushauri mambo mawili,kwanza kwa kuwa ni safari yako ya kwanza Dubai(sina uhakika)basi ifanye mwezi ujao wakati wa Ramadhani kipindi hicho ndege zinakuwa chini,hoteli zinakuwa chini na maduka mengi yanakuwa na mapunguzo ya bei.Kwa sasa hiyo pesa itatosha vizuri kununua mzigo ambao hauutumi (Shipping)ili kuepuka usumbufu wa usafirishaji na bandari bali wawezanunua vitu vidogovidogo ambavyo si vizito sana kama vifaa vya simu pamoja na simu chache au comptuter ambavyo waweza weka kwenye begi na kurudi navyo,zaidi wawezapata idea ya gharama ya vitu kwa kuangalia souq.com au awok.com japo wewe utapata kwa chini zaidi kwakuwa unachukua mzigo mkubwa.Nadhani nimekupa picha japo sijui wewe unapendelea kununua nini.
 
Last edited by a moderator:
Nafiri kwa mtaji huo ni mdogo kufanya safari ya dubai..faida yote itaishia kwenye gharama na matumizi ya safari.
 

Samahani mkuu mimi nataka kuanzisha biashara ya jewwlls(heleni,cheni,mikufu,vidani) Je gharama ya kuvitoa Dubai au china ikoje? Na jee quality ya vito vya Dubai zinalingana na vito vya china?

Samahani saana naomba msaada wako maana mie nina kiasi cha pesa kama hicho ila mimi nataka niagize na sio kufata mwenyewe huko DBI
 

Nawaona baadhi ya watu wanaofanya biz hiyo Soko la vitu hivyo ni kubwa sana,Dubai Gold Souk.Unawezapata rough idea kwa kuangalia dubaijewellers.com au ulizia info@dubaijewellers.com unawezakujua pa kuanzia
 
lucky kama unashauri mtu unadhani mtaji wa kawaida sana wa kuanzia kuchukua bishara dubai unaweza kuwa kiasi gani na biashara zipi ambazo zinaweza kumlipa kwa haraka?
 
Aksante sana kwa ufafanuzi. Ila Lucky naendelea kuuliza swali langu kama M8 ni ndogo unafikiri angejivuta mpaka kiasi gani ili aanze kufikiria kwenda dubai, na biashara gani wewe kama wewe unaona zingeweza kusaidia ku-generate income kutokana na huo mtaji kwa uzoefu zako?
 
Uko vizuri mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…