Msaada jinsi ya kupata fedha za kigeni nje ya bureau na benki

Msaada jinsi ya kupata fedha za kigeni nje ya bureau na benki

Gendaheka

Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
31
Reaction score
15
Habari zenu wakuu

Mimi ni mjasiriamali lakini kwa sasa nina wazo jipya la kufanya Foreign Exchange(Forex) lakini kwa uchunguzi wangu nilioufanya siwezi kupata faida kama nitanunua bureau na kwenda kuuza bank au bureau inayofuata

Hivyo katika uchunguzi wangu nimeona nitafute mbinu mbadala ya kupata hizo pesa za kigeni halafu nikaziuze kwenye hizo sehemu husika sasa kilichonileta hapa wadau wangu kutaka ushauri wenu ni wapi nitazipata hizo pesa na pesa ninazozihitaji hasa ni USD, GREAT BRITISH POUND, EUR na RAND pia kama itaweza kunipatia faida

Naombeni msaada ni vipi nitaweza kuwa dalali wa hizo FEDHA nionesheni machimbo yalipo wadau na mimi nikazichukue kwa bei nafuu ili nije kuuza bureau kwa bei nzuri yenye maslahi.

Asanteni sana
Nawasilisha
 
bureau na kwenda kuuza bank au bureau inayofuata hivyo katika uchunguzi wangu nimeona nitafute mbinu mbadala ya kupata hizo pesa za kigeni halafu nikaziuze kwenye hizo sehemu husika sasa kilichonileta hapa wadau wangu kutaka ushauri wenu ni wapi nitazipata hizo pesa na pesa ninazozihitaji hasa ni USD,GREAT BRITISH POUND,EUR na RAND
Hii biashara ina changamoto sana.

Bei (rate) ya wewe kununua fedha ya kigeni iko juu sana.
Na rate ya wewe kuuza iko chini sana.

Labda iwapo fedha utaito nchi moja na kuuuza nchi nyingine, lakini sio kwa hapa ndani ya nchi, kutokana na hiyo changamoto.
 
Nawezaje kujua hizo rate za nchi nyingine mkuu let say nawezaje kujua kama Kenya leo rate yao ya dollar ni kiasi flani au nchi nyinginezo ntawezaje kujua mkuu wangu?
 
Tumia simu au laptop yako kufanya hiyo biashara. Muombe Mwl.MCT akuelekeze vizuri kuhusu forex.
 
Kufanya forex manually return yake ni ndogo na risk yake ni ndogo labda uwe na mtaji mkubwa na hauwezi ukapoteza ela yote endapo direction ya soko imeenda kinyume
Ila kama unaweza kuwa na risk appetite fanya forex kwa mtindo wa margin trading ambapo mtaji mdogo unaendesha mtaji mkubwa: ila margin trading INA risk kubwa na unaweza kupoteza hela zako zote na pia return yake kubwa na unaweza ingiza faida kubwa ndani ya mda mfupi
 
Hilo ninalijua kaka ndomana nikaamua nifanye manual sasa naomba nipe muongozo jinsi ya kuanza hii manually ndugu yangu mana ndo niliyoichagua ila soko lake naona naona linabana kwa upande wa bureau na hizi bank ningependa kujua ni sehemu gani nyingine naweza kupata hizo pesa kwa bei nzuri naomba muongozo wako mkuu
 
Barclays bank umeshajaribu?
 
Sasa mkuu emb be smart bwana! Unaelekezwa njia ya kufanya bado huelewi. Huwezi kufanya biashara ya forex kati ya nchi manually kwasababu kila nchi ina muda wake wa kufungua masoko yao ya fedha. Hapo umeshaambiwa uwe na laptop/ Simu na internet full stop...Ingia kwanza ule shule za pip, traders mbalimbali kama scalper ukiweza, day, swing etc kisha kula shule za chart za trading ujue unaingia muda gani with what against what anza demo mdogomdogo then practice kwa kuweka walau usd ndogo za kuanzia...Acha papara ichukue kama kazi yako muhimu ya kwanza kabisa ipe muda wa kutosha kuwa serious fanya biashara....Ni jambo linahitaji collective ideas. Uangalifu ni muhimu na kujali pia. Sasa wewe unataka kufanya biashara ya fedha kati ya nchi na nchi manually? Hata ukijibadilisha kuwa electromagnetic waves hutaweza!
 
Back
Top Bottom