Msaada jinsi ya kupika popcorn za sukari

Msaada jinsi ya kupika popcorn za sukari

mr.piano

Member
Joined
Apr 29, 2015
Posts
11
Reaction score
3
Habari zenu wakuu, naomba mwenye ufahamu wa kupika popcorn zinazokuaga na ladha ya sukari ilitupate kufahamu hapa jukwaani kwa faida ya wengi karibuni!!
 
Unajua kutengeneza pop corn za chumvi?
Weka sukari kiasi unachotaka kwenye sufuria kavu na ubandike jikoni. Koroga taratibu huku inayeyuka. Utapata kama uji hivi wa brown. Punguza moto.

Kwenye jiko lingine tengeneza popcorn. Mahindi ya popcorn unayatia mafuta kiasi kwenye sufuria kubwa na kufunika. Yakianza kupasuka fanya kama vile unachekecha ili yaliyopasuka yapande juu.

Yakitulia mimina kwenye chombo kama sinia ama ungo. Nyunyizia sukari iliyoyeyushwa juu ya popcorn huku unazivuruga kwa mwiko ili sukari isambae kidogo kidogo.

Enjoy your movies (manake hizi shurti kwa movie lol)
 
Back
Top Bottom