Msaada jinsi ya kusave mauzo ya kila siku katika duka


Hautakiwi ubaki hata na senti tano, kila upatapo inatakiwa uongezee bidhaa mpaka ifikie uwe na bidhaa za kukuendesha mwezi mzima bila kununua nyingine.
 
Nimewahi kufanya hii biashara,nlikuwa naandika mauzo,manunuzi,na faida.nilijikuta nina faida ya ajabu kwenye daftari.ila kwenye cash mkononi hata mia,sielewi hii imekaaje???sijui ndo mambo ya chuma ulete?!!
Chuma ulete huyo
 
Habari mimi nahisi naitaji msaada wako zaidi kama utojali naomba tuwasiliane 0789566257
 
Mimi njia rahisi ya kujua faida Huwa nahakikisha kila bidhaa ninayonunua inanipa faida zaidi ya 20%,kwa hiyo huwaga kwenye kila mauzo naweka 15% kama faida ndani , Hiyo ndoo naigawanya Kodi,umeme na nyingine kujilipa mwisho wa siku.Mauzo mengine ndoo yanazunguka kwenye duka kama kawaida
 
Kiujumla duka litakupa faida pale tu mzunguko wa mauzo unapokuwa mkubwa,
Mzunguko utakuwa mkubwa pale tuutakapohakikisha mteja hakosi kitu dukani kwako
Ujanja ni kuuza vitu vyote ambavyo eidha maduka mengine Hawsuzi mfano sindano za viatu ,cherehan, za mikono,
Huu ni mfano tu Ila vipo vingi ambavyo unaweza kuwa mbunifu zaidi
Location
Ili uweze kuongeza mauzo ni lazima utafute sehemu nzuri pia yenye mzunguko mkubwa wa watu mfano wapabgaji au wapita njia wengi

Mfano
Mtaan kwangu Kuna duka linauza mauzo kwa siku laki 4 Hadi laki 8 siku za weekend
Ukiona duka lenyewe Sasa limeshona kila kitu
Na anafungu mapema na kulala kwa kuchelewa

Tuje hapa kama anauza laki 4 kwa siku anasave elfu 40 kila siku na Kodi na mambo mengine yote anatoa dukani hayahisiani na hiyo aliyotoa
Mtu kama huyo kwa mezi atakuwa na 1,200,000 kwa mwaka atasave 14,400,000
Duka ukilipenda litakupa faida kubwa sana
Shida yetu kubwa ni kuzarau au kufanya duka kama store ya familia ukiishiwa sukari unachukua tu hulipi mafuta, unga nk hivyo huwezi kuona faida
Pia tunafungua muda tunaotaka na kufunga tunavyotaka
Pia kila mtu ni muuza duka siyo dada wa kazi siyo watoto wa ndugu zako siyo baba Wala mama
Hivyo tunakosea mbona hatutumi dada wa kazi aende ofisini kwako kwa niaba yako? Au mbona huondoki kazin kabla ya muda?

Duka ni kazi kama zilivyo kazi nyinginezo
Tuliwekee mfumo maalumu wa kiuendeshaji

Ukiwa na maduka 2 na ukayasimamia vizuri utaenjoy maisha!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…