Msaada: Jinsi ya kutibu viupele vidogo vidogo kwenye ngozi ya juu inayofunika jicho

Sdebaseboy

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2015
Posts
778
Reaction score
248
Habari zenu wataalam wa afya...

Naandika uzi huu kuomba ushauri wa tiba kuhusiana na tatizo linalonisumbua. Mimi nasumbuliwa na viupele vidogo vidogo kwenye ngozi ya juu inayofunika jicho. Tatizo hili lilipoanza macho yangu yalianza kuwasha bila ya kuonekana viupele, ambapo nilienda kituo cha afya kilicho karibu kwa ajili ya kupata matibabu. Ndipo nikapewa dawa ya kufinya inayoitwa OCUCYCLINE, ambapo niliitumia bila mafanikio.

Baada ya hapo nilirudi tena kituo cha afya ambapo walinibadilishia dawa na kunipa ya maji inayoitwa IVYDEXNICOL Eye drops. Dawa hiyo yenyewe ilikua afadhali kwani nilipotumia nilidhani nimepona. Lakini kila ilipoisha na kumaliza siku 6, hali ilirudi vile vile; macho kuniwasha tena.

Ilibidi niwe nanunua dawa hiyo hiyo, kwani ndiyo ambayo ilikuwa inanipa nafuu. Miezi kadhaa baadaye niligundua kwamba kuna VIUPELE vidogo ambavyo nikijiviringa macho husababisha VIDONDA ambavyo mpaka sasa vinanisumbua.

Ninaomba ushauri, nitumie dawa gani ili niweze kupona ugonjwa huu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…