Msaada juu ya kilimo cha mahindi

kesho kutwa

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2016
Posts
1,722
Reaction score
1,965
Habari za majukumu, kama nilivyo tangulia kichwa hapo juu naombeni mwenye ujuzi wa kilimo cha mahindi anisaidie niokoe shamba langu la mahindi nimechelewa kupalilia mahindi yamebadilika rangi na kuwa ya njano, nifanye nini ili yabebe vizuri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona hakuna aneye kujibu kwa maana kuna uzi wa kilimo cha mahindi. Nenda huko watu wako active.

God save us
 
Mahindi yana umri gani? Kuna hatua yakifika basi huwezi kuyafufua tena. Kilimo kinahitaji umakini ndugu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
mahindi yanahitaji mtaji ukute hata mbolea hijaweka
 
Palilia haraka na weka mbolea ikiwepo ya SA ndani ya siku 7 utaona mafanikio.Ila usipopalilia utapoteza fedha yako
 
Kama bado hayajafikia stage ya kutoa hindi palilia na kuweka mbolea ya kukuzia(nitrogenous fertilizer) au kama shamba lako linatuhamisha maji(water lodging) tengeneza vifereji vya kutolea maji shambani fanya hayo ikiwa mahindi yapo kwenye nzur ila kama ushachelewa achana nayo kama unafuga ng'ombe tengeneza chakula cha mifugo usiingie cost ya kuhudumia shamba ambalo halitakuwa na manufaa

NB siku nyingine jitahidi kuweka pixture ili wataalam wakushauri vizuri!!!!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…