Msaada juu ya sheria na taratibu za utumishi wa umma

Adm

Senior Member
Joined
Sep 19, 2010
Posts
149
Reaction score
45
Habari wanajamvi, naomba ufafanuzi juu ya jambo hili. Mimi ni mwalimu ambaye niliajiriwa mwaka 2008 nikiwa kati ya wale walimu wa "crash program" . Baada ya kufanya kazi miaka miwili kama zilivyotaratibu za utumishi niliomba kwenda kujiendeleza,mwaka wa masomo 2011/2012 nilianza masomo udsm na nimehitimu mwaka huu.
Hivi majuzi nimechukua transcript ili nipeleke kwa mwajiri kwa ajili ya kupata tsd namba na marekebisho ya mshahara.Maswali yangu ni kuwa
1. Je nitafanikiwa kupata tsd namba nikiwa na
transcript ama mpaka niwe na cheti?
2. Kuna tetesi ambazo nimesikia kuwa siwezi
kufanyiwa marekebisho yoyote ya mshahara
mpaka nipeleke cheti je ni kweli?
3. Pia nimepata tetesi kuwa hata nikipeleka cheti
lakini itanilazimu kuajiriwa upya kama mtu
anayeanza kazi upya na wala hawata-consider
miaka niliyofanya kazi,je ni kweli?
Samahani kwa maelezo marefu, lakini naamini yatasaidia kutoa ufafanuzi wa kina. Naomba ufafanuzi juu ya hayo maswala tafadhali
 
je, unajua ofisi ya afisa utumishi wako ilipo? kama hujui, itafute utasaidiwa.
 
1. Utafanikiwa kupewa tsd namba baada ya kuwasilisha cheti (certificate) sio transcript
2.ni kwele huwezi kufanyiwa marekebisho ya mshahara hadi uwasilishe cheti (certificate) sio transcript
3.Sio kweli, ajira yako itatambulika tangu ulipoajiriwa mwanzo na ukaingizwa ktk payroll ya mshahara, kitakachobadilika ni scale ya mshahara na sio kuajiriwa upya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…