1. Mnaandikishiana kwa utaratibu ule ule kama unavyonunua kiwanja kwa mtu, panatakiwa pawepo na shahidi wa muuzaji na shahidi wa wewe unayenunua. wote mtatakiwa mtie sahihi kwenye hiyo karatasi mliyoandikishiana.
2. vitu vya msingi ambavyo unatakiwa upewe cha kwanza kabisa ni gari uliyonunua, pili documents zote za gari ikiwemo kadi ya usajili ya gari hii ndiyo muhimu zaidi na documents za rekodi ya service ya gari(kama ipo) nk.
3.Kubadili jina la mmiliki ni very simple. utatakiwa uende TRA ukiwa pamoja na original registration card ya gari pamoja na ule mkataba mlioandikishiana. kuna gharama utatakiwa kulipa ambayo itategemea na cc ya gari na bei uliyonunulia gari kutoka kwa huyo mtu aliyekuuzia. mara nyiingi kama ni gari ndogo, gharama huwa ina renji kwenye Tsh 200,000/- hadi 300,000/-.
NB: kabla hujanunua hiyo gari, mwambie anayekuuzia unahitaji kopi ya kadi ya gari, kisha nenda nayo TRA wakuangalizie kama ile gari inadaiwa au laa.
Maana huenda mwenye gari alikuwa anakwepa kulipa kodi kujanja ujanja na matokeo yake ukiimiliki wewe zigo lote litakuangukia wewe.
muhimu zaidi: Ni bora ujipige pige uagize gari kutoka japan au ununue kutoka show rooms kuliko kununua kwa mtu, UTAJUTA.
Swali lolote la ziada?