Msaada katiba ya saccos yoyote au vikoba ile.

Msaada katiba ya saccos yoyote au vikoba ile.

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
930
Reaction score
1,290
wakuu, naombeni mwenye soft copy ya katiba ya saccos au vikoba yoyote hapa bongo, kwani nataka tuanzishe vikoba au sacoss. kama mtu anayo naomba anitaarifu hapa janvini, ili mimi ni PM kwake ili nimpe email yangu anitumie. asanten kwa wote mkakanisaidia
 
Sina hakika, lakini ninadhani ulivyobandika ombi lako inakuwa ngumu kiasi kukusaidia. Ni sawa na kuomba maelezo ya kuendesha gari aina ya RAV4 au Scania kwa vile unataka kununua gari aina ya RAV4 au Scania. Yote ni magari, sawa, lakini ni yanatofauti nyingi na kubwa!

Hata hivyo, kwa sasa ushauri wangu juu ya Katiba na Taratibu za Kuanzisha SACCOS, ambao umewahi kutolewa kwa Mdau aliyehitaji Katiba ya SACCOS kama wewe siku za nyuma, ni uende ukaonane na Afisa Ushirika katika Halmashauri ya Wilaya yako. Ninaamini atakusaidia.

Kuhusu Katiba ya VICOBA (Sio Vikoba kama ulivyoandika), ngoja nipekuepekue kwenye Makabrasha yangu nione kama ninayo. Wakati nipekuapekua "search" hapa hapa JF VICOBA na au VSLA. Utapata nondo za kutosha na zaidi. Ukiona vipi, nenda kwenye Halmashauri ya Wilaya yako, Idara ya Maendeleo ya Jamii. Halmshauri nyingi hapa Nchini zina Ofisa wa Kuratibu VICOBA.

Poa!
 
Back
Top Bottom