Msaada katika tuta jamani!

Msaada katika tuta jamani!

KILITIME

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2009
Posts
265
Reaction score
18
Kwa heshima na imani kubwa sana ambayo ninayo naomba mnisaidie maana ya maneno yafuatayo na tofauti zake 1. NDOTO 2.MAONO maana yananitatiza saaana pia nawaomba mnielezee Maana halisi ya CHOTARA na je ni sahihi kuita mazao au wanyama wengine CHOTARA?????????
 
wana jf bado nahitaji msaada wenu katika hili:baby:
 
Kwa heshima na imani kubwa sana ambayo ninayo naomba mnisaidie maana ya maneno yafuatayo na tofauti zake 1. NDOTO 2.MAONO maana yananitatiza saaana pia nawaomba mnielezee Maana halisi ya CHOTARA na je ni sahihi kuita mazao au wanyama wengine CHOTARA?????????

Ndoto: (njozi, ruya): Ni mfururizo wa taswria za kimawazo na kihisia, zinazotokana na maono ya kiakili ambayo umtokea kiumbe (haswa Binadam) bila yeye mwenyewe kutaka katika hali fulani akiwa usingizini

Elimu ya utafiti wa ndoto kisayansi inaitwa oneirology.

Maono: Taswira anazo zipata mtu, akiwa usingizini au akiwa nusu kalala au nusu yupo macho au wakati mwingine akiwa macho, watu hawa wenye maono kwa kiingereza wanaitwa "psychic"

Chotara: Ni zao la (au) mchanganyiko wa wazazi wawili wenye vinasaba tofauti wanaotoka katika jamii na tamaduni tofauti. Chotara wanaweza kupatikana au kuzalishwa kutoka kwa Binadam, wanyama au mimea.

Mfano: Baba Mwenye Asili ya Afrika (Bantu) na Mama toka bara Hindi (Asia) au kinyume chake.

Mfano mzuri kwa wanyama ni Nyumbu (Mule) au kwa jina lingine Baghala, ni chotara anayepatikana kwa kupandisha Farasi na Punda.
 
Maana halisi ya CHOTARA na je ni sahihi kuita mazao au wanyama wengine CHOTARA?????????

KILITIME naona mengine Mkuu X-PASTER amekujibu vizuri tu hapo juu ... labda niongezee kidogo kwenye Chotara

shombe
nm ma- [a-/wa-] halfcaste person, mulatto, mixed blood, coloured.

chotara
nm [a-/wa-]

1. chotara = half caste, mulatto.

2. chotara = mixed breed, crossbreed (of seeds or animals):

  • Kuzaa watoto chotara = miscegenation;
  • Mbwa chotara = mongrel/mutt;
  • chotara wa Kiberiberi na Kiarabu = Moor.

miscegenation n uchotara, usuriama; kuzaa watoto chotara.
.
 
Sina hakika sana lakini nadhani tafsiri ya kwenye ndoto ndio inatakiwa iwe maono na maono iwe ndoto
ndoto ni pale ukiwa usingizini..............mabano ya njozi yanaingi pia kwenye maono......
 
"Sina hakika sana lakini nadhani tafsiri ya kwenye ndoto ndio inatakiwa iwe maono na maono iwe ndoto
ndoto ni pale ukiwa usingizini..............mabano ya njozi yanaingi pia kwenye maono......" Sijakuelewa Amavubi
 
Chotara: Ni zao la (au) mchanganyiko wa wazazi wawili wenye vinasaba tofauti wanaotoka katika jamii na tamaduni tofauti. Chotara wanaweza kupatikana au kuzalishwa kutoka kwa Binadam, wanyama au mimea.

Je mnyemwezi na mngoni wakizaa mtoto wao atakua chotara????
 
Je mnyemwezi na mngoni wakizaa mtoto wao atakua chotara????
Ukipenda unaweza kumwita mtoto chotara wa Kingoni na Mnyamwezi, lakini mara nyingi wanaangalia Asili ya wazazi, na haswa asili kwa maana ya Race badala ya Ethnic, sababu kabila zote hizo ulizo zitaja ni Wabantu.

Labda ungeuliza kati ya Mmasaai na kabila lingine la Kibantu... Maana Wamasaai inasemekana asili yao hasa ni KaskaziniMashariki ya Afrika (Cush au Kush/Habasha au Abyssinia) , ambayo ni kuanzia Somalia mpaka Ethiopia ya leo.

Kama kuna wataalam zaidi wanaweza kuchangia katika ili.
 
Back
Top Bottom