Pole mkuu, kwanza utaratibu wa kuteua msimamizi wa mirathi sijui kama ulikuwa sawa. Ninavyojua mimi akifa mmoja wa wazazi basi anayebaki ndo msimamizi wa mirathi. Mama yako bado yupo? Kama yupo basi kihalali ndo msimamizi wa mirathi, kama hayupo basi watoto wenyewe ndo mnateua msimamizi wa mirathi miongoni mwenu, huyo aloteuliwa ni mwangalizi wa familia tu kimila na si msimamizi wa mirathi nadhani terms hapa ndo zilikosewa, kama waliandika hivyo basi mnaweza kwenda mahakamani kufungua jalada la kubadili msimamizi wa mirathi na kumteua mwingine. Kimsingi ndugu wa karibu hawahusiki na mirathi isipokuwa watoto na wazazi.
Mimi nilifiwa na mzazi wangu wa kiume ambaye alikuwa mwajiriwa serikalini. Baada ya mazishi kikao cha wanandugu kilimteua baba mdogo kama mfuatiliaji wa mirathi. Lakini tangu kuteuliwa kwake huyo baba mdogo hafuatilii waa haonyeshi juhudi zozote. Swali kwenu ndugu zangu wana jf,SHERIA INASEMAJE KUHUSU KUMBADILISHA MSIMAMIZI WA MIRATHI ENDAPO ALIYEPO HAONYESHI KUWA ACTIVE? Naombeni msaada kwa hilo kwa mwenye uzoefu wa kesi hiyo ama mwenye ufahamu wa sheria juu ya hilo
Baada ya mazishi kikao cha wanandugu kilimteua baba mdogo kama mfuatiliaji wa mirathi. Lakini tangu kuteuliwa kwake huyo baba mdogo hafuatilii ...
Kwa mujibu wa suala lako, Unayo haki kisheria kama mmoja wa warithi kwenda mahakamani pale pale mlipofungulia mirathi yenu na kuweka pingamizi kwa msimamizi w mirathi na kutoa sababu zinazokufanya usiridhike na utendaji wa huyo msimamizi.( kuna fomu maalum utajaza kisha mtapangiwa siku ya kusikilizwa pingamizi lako na kama litakubaliwa basi Mahakama itatengua uteuzi wa huyo msimamizi wa mirathi na hivyo mtatakiwa kuchagua msimamizi mwingine.
Hivyo hiyo ni haki yako, nenda mahakamani kaweke pingamizi na utoe sababu za pingamizi lako za kutoridhishwa na utendaji wa msimamizi wa mirathi yenu.
umeongea vyema sana. pia waweza kubofya hapa kwa wale wanaohitaji vitabu. SHERIA TANZANIAUnachokisema sio sahihi kabisa.
Kwa mujibu wa Sheria za tanzania, msimamizi wa mirathi ambaye anatambulika kisheria ni yule ambaye mara baada ya kifo cha marhum basi ndugu wote waliomuhusu ikiwemo pamoja na warithi wataakaa kikao chenye ajenda ya kuchagua msimamizi wa mirathi.
Mkutano huo utakuwa na mwenyekiti na katibu wa kuratibu na kuandika muhtsari na muhudhuriaji atatakiwa kutia sahihi muhtasari huo. ndani ya kikao hicho atachaguliwa msimamizi wa mirathi naye atapitishwa na wajumbe wote kisha nakala ya muhtasari huo utapelekwa mahakamani na picha na death certificate na ushahidi mwingine na kuomba mahakama imthibitishe kisheria kama yeye ni msimamizi halali wa mirathi ya marehemu yule.
Msimamizi anaweza kuwa mama, Mtoto akiwa na zaidi ya umri wa miaka 18 and ndugu yeote atayechaguliwa na kikao hicho.