Msaada: Kiasi gani cha Kodi hulipwa TRA kama utaka kufungua Consultant Firm?

mwanawao

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2010
Posts
3,192
Reaction score
5,743
Wakuu, Heri ya mwaka mpya. Please naombeni kufahamu kodi inayotakiwa kulipwa TRA kama unataka kufungua Consultant Firm. Nina imani wapo wengi ambao ama wanafanya shughuli hii au wana uelewa na hii kitu naombeni msaada wenu.

Wapo wengi watakaouliza mbona usiende TRA kupata taarifa? Nimeona ni vyema kuwa na information kwanza kabla ya kwenda huko maana ninaweza kwenda kichwa kichwa nikapigwa kodi ya ajabu.

Natanguliza shukrani zangu kwa msaada wenu..
 
Mkuu mbona usha jijibu wewe nenda TRA utapata kila kitu, Kuna kitengo cha Elimu kwa walipa Kodi utapata hadi Vitabu vya kuleza jinsi ya Kulipa kodi, na TRA c wenda wazimu kwamba wakukadirie kodi ya Juu, na hata hivo TRA hukadiria watu kwa sababu watu huficha baadhi ya Information but ukiwa unaendesha Biashara yako kisasa na mahesabu ako yana be Audited hutakadiriwa hata siku moja bali utalipa kile kilichopo
 
Thanx chasha kwa ushauri ntafuatilia
 
Naamini hiyo consultant firm utaifungua kama kampuni si ndio?
Nyingi ni kampuni hivyo hata siku moja TRA huwa hawaikadilii kodi kampuni, Auditor/accountant wa kampuni ndiye anayekadiria kodi ya kampuni na kuwasilisha makadirio hayo pale TRA.
Kitendo hicho ni cha lazima kwa mujibu wa sheria ikitokea kampuni imekiuka hapo ndipo TRA itakukadilia plus fines and interest.
Kama unafungua hiyo firm as individual basi utakadiriwa kodi hapo hapo TRA pia waweza kujikadiria mwenyewe ila ni lazima makadirio hayo yahakikiwe na Certified Accountants utaemchagua wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…