kiria babu
Member
- Sep 13, 2017
- 12
- 8
Nilimpa kijana pikipiki yangu awe anafanyia kazi ya bodaboda ile siku namkabidhi pikipiki ile usiku wake nikapata ajali hivyo ndugu yangu alipoteza maisha katika ajali hiyo wakati nikiwa ICU, kijana niliyempa pikipiki ile alipiga simu akaongea na ndugu yangu akidai ameibiwa pikipiki na hapohapo yupo namdhamini aliyemwaminisha awape pikipiki mabwana wale wakaamishe kitanda hivyo akawapeleka kituoni polisi na kuwafungulia mashitaka ya wizi wa kuaminiwa wakalala police asubuhi yake walipewa dhamana.
Nilipopona nikaenda kituoni pale kuwaeleza nikaambiwa kesi ishafunguliwa hivyo hatufungui kesi mbili nikamuuliza mimi ni mwenye mali na nina vigezo vyote kadi nk... hivyo aliyefungua kesi ile ni mtuhumiwa kwangu hivyo hastaili kufungua kesi bali anatakiwa anipe ushirikiano na wenzake wa kupata mali yangu.
Yaani mpaka sasa sijamuelewa mpelelezi wa kesi ile aseee maana nikiiitaji mrejesho hanipi wala hataki kuulizwa chochote. Nishauri wenzangu.