Msaada: Kila nikiamka asubuhi kichwa kinauma

Msaada: Kila nikiamka asubuhi kichwa kinauma

Bakulutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2011
Posts
2,557
Reaction score
1,787
Habar JF Dk,
Kila niki amka asubuhi kichwa kinauma, kiasi kwamba naweza shinda nacho au kikatulia mchana.
Maleria sina.
 
cheki mazingira unayolala kukosa hewa ya kutosha pia ni tatizo,au kama unalala kwa kutumia feni yani pangaboi huwa inakelele flani inayoumiza kichwa pole sana.ila subiri maoni mengine ya kitaalamu zaidi
 
Mkuu, msaada wako ni mkubwa saana ngoja niufanyie kaz mapema...
 
Kunywa maji unapoamka! Anza an kiasi kidogo!
Tatizo ni kwamba anapolala hapana oxygen ya kutosha. Wala halina uhusiano na kunywa maji asubuhi. Ajitahidi kama anaishi kwenye nyumba zenye gypsum na alminium kiasi cha kwamba hakuna hata tundu la kutolea hewa, basi afanye mpango wa kufungua madirisha usiku akilala. Kuna mmoja hapo juu kasema kuhusu feni. Nakubaliana pia, feni huwa ina tabia ya kuondoa hewa, safi iliyo karibu na wewe, na kuleta yenye impurities. Haishauriwi kulala na feni ikiwa inafanya kazi ni marufuku pia kumuwekea feni mtoto mdogo.
 
Ok...Mimi nimepost kulingana na experience yangu. Ila kwa swala la hewa mm huwa siwezi kulala chumba kilichofungwa, lazima niache mlango au dirisha wazi. Kuna kipindi pia iwepo nimepigwa sana na jua, hasa katika kusubiri daladala au hata kwa kukaa dirishani, kichwa kinagonga hata siku mbili na tiba ni maji kwa wingi!.
 
Unachokisema ni sahihi kabisa. Mimi nina zaidi ya miaka kumi sasa sijawahi kunywa panado kwa ajili ya kutibu kichwa. Matibabu yangu makubwa ni maji. Hata hayo maji ya asubuhi pia kwangu ni routine, lakini huwa hayasaidii pale unapokuwa umeamka na maumivu ya kichwa yatokanayo na kukosa hewa. Utakunywa, lakini utaendelea kuumwa kichwa hadi baadaye mchana baada ya kuwa exposed kwenye oxygen ya kutosha.

Kwa hiyo pamoja na maji, cha kufanya ni kujitahidi kupata hewa ya kutosha. Hili nimeliandika kutokana uzoefu wangu mimi mwenyewe. Nilishakuwa na tatizo kama analolielezea huyu jamaa, na nilishajaribu matibabu ya maji hayakunisaidia, hadi nilipoanza kufungua mapazia usiku ninapolala.
 
Habari wakuu,

Sijui nina tatizo gani. Kwa muda sasa, nimekua kila siku nikiamka asubuhi kichwa kinaniuma. Naomba msaada kwa anayeelewa hii hali. Asante.
 
Kapime pressure, na huenda unaota ndoto mbaya mbaya sana.
 
Poleee mkuuu .unywee na majii mengiii itakusaidiaa piaa maumivu yakizidi mwone daktarii
 
Jaribu kucheki kipanda uso. For a time being jaribu kutumia dawa za typhoid aina ya Cipro! I believe itakusaidia.

Nimewahi kuwa na shida kama yako, baada ya kutumia dawa hizi nilikuwa najisikia kupata nafuu. Nikiacha nasikia mwili umechoka na kichwa kuuma. Tatizo lilikuja kuisha lenyewe... Jaribu kwanza utanipa feedback.
 
Kabla ya kulala jitahidi unywe nusu lita ya maji,na mazingira unayolala hakikusha ni safi na tulivu. Pole mdau
 
Habari wakuu,

Sijui nina tatizo gani. Kwa muda sasa, nimekua kila siku nikiamka asubuhi kichwa kinaniuma. Naomba msaada kwa anayeelewa hii hali. Asante.

Mimi kila nikiamka asubuhi m*oo inadinda ;naomba msaada wenu kwa anaeelewa tatizo hili.asante.
 
Mkuu hulewi lkn, zaidi hapo kamuone daktari hiyo ndio njia muafaka hapa (JF) wengi ni wanasiasa watakuzinguwa tu.
 
Back
Top Bottom