Msaada: Kila ujauzito wa mke wangu unapofikisha miezi mitatu na kuendelea, anatokwa na damu puani

Msaada: Kila ujauzito wa mke wangu unapofikisha miezi mitatu na kuendelea, anatokwa na damu puani

Norshad

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2013
Posts
5,211
Reaction score
12,538
Asallam aleykum, ndugu zangu..
Mimi nina tatizo, na tatizo hili lanamsibu Mke wangu,

Mkewangu kila apatapo ujauzito ifikapo miezi mitatu na kuendelea huwa anatokwa na damu puani, leo hii pia hali hiyo imejirudia, naomba msaada kwa yoyote anayefahamu hili tatizo na suluhisho lake anifahamishe.

Natanguliza shukrani
 
Asallam aleykum, ndugu zangu..
Mimi Nina tatizo, na tatizo hili lamsibu Mkewangu, Mkewangu kila apatapo ujauzito ifikapo miezi mitatu na kuendelea huwa anatokwa na damu puani, Leo hii pia hali hiyo imejiridia, naomba msaada kwa yoyote anayefahamu hili tatizo na suluhisho lake anifahamishe.

Natanguliza shukrani
Mkuu pole kwa kuuguza.. Tambua mimba zina mambo mengi lakin binafsi nakushaur umpeleke hospital akaonane na matabibu , usisubir mpaka uje uambiwe. Its too late...
 
Ni kweli hospital ntampeleka, tena kesho tu inshaAllah lakini niliamini humu pia naweza pata msaada wa ki mawazo
 
Inshaallah ahsante kaka ntafanya hivyo, sababu ya kuomba ushauri ni hii, hii si mara ya kwanza ujauzito wa kwanza hii hali alitokea na tukaenda hospital, hali hii haikukata mpaka alipojifungua ndipo iliacha kabisa, na sasa imejirudia baada ya kushika ujauzito mwingine
 
Hospitali ndo unapata majibu ya maana zaidi kuliko humu
Mkuu kama hujuwi tiba yake ni kukaa kimya kwani mleta mada hajuwi kuwa kuna hospitali? Kama huna jibu la kujibu bora unyamaze ili watu wengine tunao juw atiba tupate kumsaidia mwenzetu sio kuleta ubishi usio na maana samahani kama nimekukwaza.
 
Asallam aleykum, ndugu zangu..
Mimi Nina tatizo, na tatizo hili lamsibu Mkewangu, Mkewangu kila apatapo ujauzito ifikapo miezi mitatu na kuendelea huwa anatokwa na damu puani, Leo hii pia hali hiyo imejiridia, naomba msaada kwa yoyote anayefahamu hili tatizo na suluhisho lake anifahamishe.

Natanguliza shukrani
IFAHAMU NJIA HII YA KUZUI DAMU KUTOKA PUANI

IFAHAMU NJIA HII YA KUZUI DAMU KUTOKA PUANI.jpg


Matukio ya kutoka damu puani mara nyingi hujitokeza kwa baadhi ya watu , tatizo hili mara nyingi husababishwa na mipasuko midogo ya mishipa ya damu ndani ya pua inayosababishwa na kujeruhiwa au hali ya msukumo wa juu wa hewa , mzio (allergies) wakati mwingine huwa ni madhara yatokanayo na madawa.

Kwa ujumla tatizo hili huwa halina maelezo kamili ya chanzo chake, lakini watu wenye msukumo wa juu na wa chini wa damu huwa na nafasi kubwa ya kupata tatizo hili.

Moja ya tiba ya kuzui kutoka kwa damu puani ni pamoja na majani/ mbegu za embe. Tiba hii ni kutengeneza juisi ya majani ya mbegu ya embe kisha mgonjwa atatakiwa alazwe chali kisha weka matone matano ya juisi hiyo katika kila pua.

Hali kadhalika nusu glasi ya juisi ya majani au mbegu ya embe inaponywewa ni dawa nzuri ya kuzuia kutoka damu puani.http://www.dkmandai.com/2015/03/ifahamu-njia-hii-ya-kuzui-damu-kutoka.html


 
lakini si anajifungua salama kabisa,,,,,,,,kama inaleta shida had kwa mtoto better to see the doctor
 
Back
Top Bottom