Napenda sana kilimo cha zabibu, hata kama sio kwa shamba kubwa basi iwe kidogo tu kwa ajili ya matunda, lakini kwa hapa Tanzania huwa naona zinastawi sana Dodoma.
Sasa kwa wale wataalam wa kilimo naomba mnifahamishe kama naweza kuwa na shamba la zabibu Dar es salaam na zikastawi. Je hali ya hewa inaruhusu?
Najua wapo watakaoniambia niende google lakini mi ningependa kusikia kwa wataalam wa hapahapa nchini.
wakuu, ninajiandaa kuingia kwenye kilimo cha zao hili kwa kuwa mipo eneo ambalo zao hili linastawi(dodoma).. lakini sipo eneo ambalo lipo karibu na wazalisaji wa zao hili watakao nisidia kulifahamu vizuri zao hili...sasa kwa wenye taarifa na ujuzi kuhusu zao la zabibu naomba wanijuze pia kwa faida ya wengi ili nijue naanzia wapi na naanza na nini
=================================
mapenz matam post:
MUONGOZO WA KILIMO CHA ZABIBU KIBIASHARA
UTANGULIZI
Kitabu hiki kinatoa muongozo wa mbinu bora za uzalishaji wa Zabibu kwa mkulima wa kawaida,pia tumetumia lugha rahisi ili kumuwezesha mkulima kuelewa kwa urahisi,na pia kimetumia michoro mingi ili kumsaidia mkulima kuona kwa vitendo,na pia kimetumia mazingira halisi ya Wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma.
Jitihada nyingi zimefanyika ili kuhakikisha Wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma wanalima kisasa zaidi ili kujihakikishia mavuno bora na ya uhakika kipindi cha msimu wa mavuno.
Kutokana na utafiti uliofanyika na Taasisi mbalimbali inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya Wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma wanalima kutumia uzoefu tu na si kitaalamu kama inavyotakiwa,hii inapelekea Wakulima wengi kutumia gharama kubwa katika uzalishaji wa zao hili kwa kuwa wengi wao wanatumia uzoefu na siutaalamu,hivyo kupelekea Wakulima kupata kipato kidogo ambacho hakilingani na uwekezezaji walioweka.
Hivyo kitabu hiki kitaainisha mbinu zote za msingi katika uzalishaji wa Zabibu ili kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji,na pia kuendesha kilimo kibiashara zaidi.
Nimatumaini yangu kuwa kama Wakulima watazifuata mbinu hizi wataongeza uzalishaji wa zao hili na hivyo kuwaongezea kipato zaidi.
SURA YA KWANZA
1:0 HISTORIA YA KILIMO CHA ZABIBU KWA UFUPI
Kilimo cha Zabibu mkoani Dodoma kina historia ndefu, ambapo kwenye miaka ya 1950 na mwaka 1974 chini ya uzaidizi wa bihwana misheni, serikali ya Tanzania wakati huo ikishirikiana na serikali ya china ilianzisha kituo cha kilimo cha Bihawana Farmers Training Center (BFTC) kwa ajili ya kufundisha Wakulima juu ya kilimo cha Zabibu na mazao mengine.
Wakulima wengi walijifunza mbinu mbalimbali juu ya kilimo cha Zabibu na wengi wao walianzisha mashamba ya Zabibu. Na katika miaka ya 1990 kilianzishwa kiwanda cha mvinyo cha DOWICO,kiwanda hiki kilisababisha Wakulima wengi waingie kwenye kilimo cha Zabibu.
Katika miaka hiyo ya 1990 viwanda vya mvinyo viliongezeka na Wakulima wengi wakaanza kuanzisha mashamba ya Zabibu ili kuvilisha viwanda hivyo,.
Dodoma ndio mkoa pekee unaolima Zabibu kwa wingi nchini Tanzania na hata kwa afrika mashariki ndio mkoa wenye utajiri mkubwa wa zao hili.Hii pekee ni fursa kwa wananchi wa Dodoma katika kulitilia mkazo zao hili ili liweze kuinua uchumi wa wananchi wa mkoa huu.
Kijitabu hiki cha kilimo bora cha Zabibu kimeeleza kwa undani juu ya mbinu zote za kilimo cha Zabibu kuanzia kujua aina ya udongo,uandaaji wa shamba,maji,magonjwa,uvunaji,aina za Zabibu n.k napia kimeangazia muelekeo wa kilimo cha Zabibu kibiashara zaidi.
1:1 Ukweli kuhusu kilimo cha Zabibu
Katika kiini chake kilimo ni utatuzi wa changamoto mbalimbali,kwahiyo kama hutajiweka kama mtatuzi wa changamoto hizo ni bora uachane na kilimo. Kila siku shamba la Zabibu litakuletea changamoto mbali mbali ambazo itakubidi uzikabili,
Je, unawezakipindi cha mvua kukabiliana na magugu,unaweza ukapalilia leo baada ya siku tatu yakaota mengine, hali kadhalika kipindi cha mavuno kinapokaribia kuna changamoto ya ndege wanaokuja kuharibu Zabibu na hao pia unabidi ukabiliane nao, Je uko tayari?
Nimejaribu kukuelezea haya sio kwamba nataka nikuogopeshe la hasha!ila ni kukuweka katika picha ambayo itakusaidia kujua hali halisi ya kujua majukumu utakayoenda kukabiliana nayo pindi utakapoingia katika kilimo hiki.
Swali la msingi hapa ni kwa namna gani utalima Zabibu katika vipindi vyote vya masika,kiangazi n.k katika vipindi vyote hivi kuna magonjwa kulingana na hali ya hewa ya kipindi husika.
SURA YA PILI
1.1 Maeneo yanayolimwa Zabibu mkoani Dodoma
Hali ya hewa ya Dodoma inaruhusu zao hili kustawi katika maeneo mengi mkoani hapa,baadhi ya maeneo yanayolimwa Zabibu ni Mpunguzi, Mbabala, Hombolo, Chamwino, Bahi, Mvumi, Msalato, Gawaye .
Kwa asilimia kubwa maeneo haya yanategemea mvua na kwa baadhi ya maeneo wanatumia mifumo mbalimbali ya umwagiliaji mfano Hombolo wanatumia mifereji inayopitisha maji kutoka bwawa la Hombolo,Chamwino wanatumia umwagiliaji wa matone.
Ramani ya mkoa wa Dodoma: uzalishaji mkubwa unafanywa katika wilaya ya Dodoma mjini, ikifuatiwa na chamwino na Bahi.
SURA YA TATU
3.0 HATUA KUMI ZA KUANGALIA KABLA HUJAANZISHA SHAMBA LA ZABIBU
Kumekua na wimbi kubwa kwa watu wanaofanya kazi za maofisini kuingia kwenye kilimo hiki hasa wakijua kua kilimo hiki kina tija katika kujikwamua kiuchumi,nah ii imepelekea hata wale Wakulima wazoefu na wenyewe kuongeza mashamba yao,huku wakiamini kuwa ipo siku zao hili litarudisha Heshima yake ya miaka ya tisini,kwakua sasa Zabibu inalimwa na watu wa kada tofauti tofauti. Hivyo basi kabla hujaamua kuingia kwenye kilimo hiki au kupanua shamba lako hebu jaribu kupitia hatua hizi ndipo ufanye maamuzi sahihi.
1. Kwanza unatakiwa uangalie kuwa unalenga soko lipi, je ni kwa wenye viwanda? Au wanunuzi wadogo wadogo?kama ni kwa wenye viwanda inabidi ujaribu kuongea nao kwanza uone mtazamo wao na ni aina ipi ya Zabibu wanazihitaji.
Ni wazo zuri pia kama utapata mawasiliano ya uhakika na wenye viwanda ikibidi kama watakuhakikishia kuingia mkataba nao mara utakapoanza uzalishaji.
2. Pili inabidi ujue nini unakifanya,hapa namaanisha ujuzi wa zao hili, wengi wa Wakulima wanaolima zao hili kwasasa hawana utaalamu wengi wao wanatumia uzoefu tu. Sisemi kwamba wanafanya vibaya ni kitu kizuri kutumia uzoefu lakini ukiongeza na ujuzi kidogo inakua ni kitu kizuri zaidi, maana utajua nini unafanya katika kilimo hiki.
3. Tatu fanya utafiti binafsi kwa kuongea na Wakulima wazoefu ili kujua ni aina gani ya Zabibu inastawi katika eneo husika, pia kuna mabwana shamba ambao wana utalaamu juu ya kilimo hiki cha Zabibu nenda kaongee nao uone wanakushauri nini. Pia ni vyema ukazalisha Zabibu ambazo wenye viwanda vya mvinyo wanazihitaji wao ni soko la uhakika.
4. Nne kama mipango pia nikuanzisha kiwanda cha mvinyo ili Zabibu utakazolima uzipeleke kiwandani kwako. Nivyema ukafanya utafiti juu ya Masoko ya mvinyo utakaotengeneza,ujue wateja wako ni kina nani wanapendelea mvinyo wa aina gani n.k
5. Uwe na mtaji wa kutosha utakaokuwezesha kuishi kwa miaka mitatu hadi mitano bila kutegemea kipato chochote kutoka kwenye shamba lako la Zabibu, maana Zabibu itaanza kukulipa kuanzia mwaka wa tatu na kuendelea.
6. Sita hakikisha unaanzisha shamba kwenye udongo sahihi unaoendana na uzalishaji wa Zabibu, udongo ndio kitu cha msingi kabisa kuzingatia kabla hujaamua kuanzisha shamba la Zabibu.
7. Saba anza na ekari chache hii itakusaidia uendelee kujifunza taratibu juu ya kilimo hiki kwa vitendo huku akili yako ikiwa imetulia,usianze na uwekezaji mkubwa maana utakupa changamoto kwa kuwa ndio mara yako ya kwanza kuanza kilimo hiki.
8. Nane, tafuta mkulima mzuri na mzoefu mwenye shamba zuri la Zabibu, au jiunge na vyama vya Wakulima wa Zabibu kama UWAZAMAM, MBABALA, GAWAYE N.K hapa utapata fursa ya kujifunza kwa vitendo namna wenzio wanavyolima Zabibu na namna wanavyokabiliana na changamoto mbalimbali za zao hili.
9. Jaribu kujifunza namna bora ya ukatiaji wa Zabibu,katika kilimo hiki cha Zabibu ukatiaji ndio kiini cha uzao wa Zabibu,ukikosea katika ukatiaji unaweza usipate mazao kwa msimu mzima. Hivyo ni muhimu ukajifunza namna bora ya ukatiaji wa mizabibu. Utaelewa kwa kina juu ya ukatiaji katika sura zinazofuata za kitabu hiki.
10. Kumi ,uwe na mtazamo wa kulima kibiashara zaidi, usilime Zabibu kwa mazoea,lima zao hili huku ukiamini kuwa hii ni kazi yako usilime kama kazi ya ziada tu. Ongeza juhudi na maarifa katika kilimo hiki.
Nimeamua kukuwekea hatua hizo kumi za kufuata kabla hujaanzisha shamba la Zabibu,hata kama tayari umeanzisha shamba la Zabibu jaribu kuzipitia hatua hizo uone kama ulizipitia au la,japo nimatumaini yangu kuwa kuna baadhi walizipitia hata kama sio zote.
3:1 AINA YA ZABIBU
Kwa ujumla kuna aina tatu za Zabibu ambazo ni Zabibu za mvinyo,Zabibu za mezani na Zabibu za kukausha ambazo zote zinazalishwa mkoani hapa. Zabibu zinazozalishwa kwa wingi mkoani hapa ni mvinyo zikifuatiwa na za mezani.
Aina zote hizo nilizozitaja hapo juu zimegawanyika katika makundi tofauti tofauti mfano Zabibu za mvinyo zimegawanyika katika makundi mawili ambapo kuna Zabibu nyekundu maalumu kwa ajili ya kutengenezea mvinyo mwekundu na kuna Zabibu nyeupe kwa ajili ya kutengenezea mvinyo mweupe.
3:2 HALI YA HEWA
Zabibu haihitaji mvua nyingi, maeneo yenye mvua za wastani ndio yanafaa kwa kilimo cha Zabibu mfano Dodoma, unaweza ukajiuliza kwanini Dodoma ni pakame lakini ndio wazalishaji wakubwa wazabibu Afrika mashariki! Pia ardhi ya Dodoma ina hifadhi maji kwa kipindi kirefu mfano kwa mvua zinazonyesha kuanzia Desemba mpaka Machi zinatosha kabisa kuhudumia mizabibu mpaka mwezi wa Julai kwa mavuno ya kiangazi.
Hali hii ya Dodoma ndio inayofanya Zabibu yake kuwa bora kuliko sehemu yoyote ile Afrika Mashariki,zina kiwango kikubwa cha sukari, pia unaweza ukazihifadhi kwa muda mrefu kidogo,zina ganda gumu ukilinganisha na Zabibu za sehem nyingine.
HATUA ZA KUFUATA WAKATI WA UANZISHWAJI WA SHAMBA LA ZABIBU
Kabla ya kuanzisha shamba la Zabibu kuna hatua kumi za msingi za kuzifuata kwa mpangilio,ili kuweza kuleta tija katika uzalishaji wa Zabibu.
1. Kufanya utafiti juu ya aina ya udongo unaofaa katika uzalishaji wa Zabibu, katika utafiti niliofanya nimegundua Wakulima wengi hawafanyi utafiti juu ya udongo unaotakiwa katika uzalishaji wa Zabibu.
Udongo unaofaa kwa kilimo cha Zabibu kwa hali ya hewa ya Dodoma ni mchanganyiko wa mfinyanzi, kichanga na tifutifu, hata kama utapata mahali ambapo udongo huu wa mchanganyiko haupatikani itabidi uchimbe mitaro na unapochanganya mbolea itabidi uchanganye na aina hizo za udongo.
Moja ya faida ya aina hiyo ya udongo ni kuwa inasaidia mizizi ya mzabibu kujitawanya kwa nafasi,na pia hewa na maji vinapata nafasi kwa urahisi.
Picha: katika picha hii utaona jinsi mizizi ya Zabibu inavyojitawanya kwa nafasi kwa kua udongo huu Ulichanganywa vizuri na hivyo kuacha nafasi kwa mizizi kujitanua kwa urahisi.
2. Kuandaa mitalo kufuatana uelekeo wa jua linapotokea, unapoandaa shamba la Zabibu inabidi mistari ya mitalo uchore kufuatana na jua linapochomoza, moja ya faida ya kuangalia uelekeo wa jua ni kwamba chakula cha mmea kinatengezwa kwa nguvu ya jua pia, hivyo inakupasa kuangalia kigezo hicho ili kuweza kupata mimea yenye afya na uwezo wa kuhimili mazao yatakayo zalishwa, Zabibu inahitaji jua la kutosha ili kuweza kuzalisha chakula cha kutosha kwa mimea yake. Chimba mitalo yako na uhakikishe angalau inapata jua kwa asilimia 80.
Mitaro ya Zabibu kufuatana na ulekeo wa jua,mashariki kwenda magharibi kufuatana na picha hii
3. Kuhakikisha unapata miche bora ya mizabibu,hapa kuna Wakulima wana vitalu vyao na kuna wengine wananunua kwa Wakulima binafsi au kwa taasisi zinazojishughulisha na Zabibu mfano Makutupora kituo cha utafiti. Miche bora ya Zabibu ndio itakayo kuwezesha kupata mazao ya uhakika mbeleni, na ndio maana tunashauri Wakulima wanunue miche bora iliyoandaliwa kitaalam.
Wakulima wengi mkoani hapa wanategemea makato ya miche kutoka kwenye mashamba yao kitu ambacho sio sahihi sana maana kunakua na mzunguko mkubwa/mrefu uzao,na pia Wakulima wengi wanashindwa kuchagua makato yenye ubora nah ii hupelekea kukosa mazao ya uhakika.
Picha namba 3, makato ya Zabibu yaliyoandaliwa katika ubora wa hali ya juu,yakisubiri kuchipua
Picha namba 4,Muonekano wa kitalu kilichoandaliwa vizuri
4. Kuanda mitalo kabla hujahamishia miche shambani, hii ni hatua muhimu na Wakulima wengi hushindwa katika hatua na kujikuta wanaharibu miche mingi shambani mara tu baada ya kuihamishia maana miche huungua kwa kuwa wanashindwa kuchanganya kwa wastani mzuri mbolea na mchanga, unashauriwa katika kila kilo moja ya ya mbolea/samadi unachanganya mchanga robo kilo, na baada ya kuchanganya unatakiwa ufukie mitaro yako kwa muda wa mwezi mmoja au miwili ili kuacha mbolea ioze vizuri na kuiacha ardhi ikiwa na rutuba ya kutosha, pia tunashauri Wakulima wanaoandaa mashamba/mitalo mipya kuiandaa kuanzia mwezi November ili mvua zitakazoanza desemba zikute umeshafukia mitalo yako vizuri na kuozesha mbolea kwa haraka zaidi.
Udongo uliochanganywa vizuri na samadi mitaro iliyoandaliwa vizuri kwa nafasi
5. Kuhamishia miche kutoka kwenye kitalu na kuhamishia kwenye shamba lililoandaliwa vizuri,usije ukahamishia miche kwenye shamba ambalo halikuandaliwa vizuri maana itakugharimu hutapata matokeo mazuri baada ya muda kupita.
Kabla ya kuanza kuhamisha miche kwenye shamba inabidi uhakikishe kuna maji ya kutosha maana kila mche unatakiwa uwe kwenye unyevu ili kuzoea maisha mapya ya shambani.pia ni vyema Wakulima wazingatie nafasi kati ya mche na mche na mtaro na mtaro
Shamba liloandaliwa vizuri tayari kuhamisha miche,hapa ndipo miche hii itamalizia masiha yao hapa hivyo ni vyema eneo liandaiwe vizuri.
6. Baada ya miche ya Zabibu kuhamishiwa shambani katika hatua hii, mkulima inakupasa kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha hakuna mmea unaokufa ama kwa ukame au kuliwa na wadudu.uzoefu unaonesha kuwa Wakulima wengi wakishahamishia miche shambani wanajua washamaliza kazi,hivyo ni vyema kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kujua maendeleo ya miche yote.
Mmea wa mzabibu wenye afya nzuri na ambao unafuatiliwa kwa ukaribu sana
7. Baada ya miche kushika vizuri, itaanza kustawi na kuonesha dalili za kutambaa, hivyo basi hichi ni kipindi cha kuanza kuifundisha namna ya kutambaa kwa kutumia kamba na fito nyembamba.
Picha hizi zinaonesha ni namna gani unaweza kufundisha mmea wa Zabibu namna ya kutambaa kwenye wire na fito
8. Baada ya kuufundisha mmea wa Zabibu,kinachofuata ni ukatiaji wa mzabibu,katika hatua hii hapa ndipo unaundaa mmea wako kwa ajili ya uzao,bila kukatia huwezi kupata mazao.
vifaa vinavyotumika kwa ukatiaji ni kama mkasi, msumeno n.k..kuna aina mbili za ukatiaji wa mizabibu ambapo kuna Dodoma cordon ambao utakuwezesha kupata mazao kwa misimu miwili,na southAfrican type of pruning (ukatiaji wa kia Afrika kusini) ambao utakuwezesha kupata mazao kwa msimu mmoja.
Vifaa vya ukatiaji
namna ya ukatiaji
9. Hatua inayofuata ni uzaaji wa mizabibu iliyokatiwa vizuri,kama ulivyoona katika hatua namba nane kuwa ukatiaji ndio unaosababisha mzabibu kuzaa,na pia ubora wa matunda.
Hatua inazopitia mmea wa mzabibu toka kukatiwa mpaka kuzaa matunda yenye ubora
10. Moja ya mambo ambayo yamekua ni changamoto kubwa wakulima wengi ni Wadudu na magonjwa ya mizabibu. Magonjwa pamoja na wadudu waharibifu wanaweza kuchangia kupata hasara hadi ya asilimia 100. Baada ya kuandaa shamba, kununua miche na kupanda miche yako, kazi kubwa inakua ni utunzaji wa mizabibu yako. zabibu ni moja ya mazao yanayopendelewa sana na wadudu na magonjwa, hivyo inahitajika umakini wa hali ya juu sana. Kwanza tunachotakiwa kufahamu ni kwamba Zabibu inahitaji ufuatiliaji wa karibu sana.
Kuna vitu viwili hapa naomba nivieweke sawa
- Kuna kinga dhidi ya mzabibu –ambapo kuna dawa kwa ajili ya kinga
- Kuna kutibu mzabibu baada ya kupata ugonjwa-kuna dawa zake pia
Kitu ambacho Wakulima wengi hawafuatilii ni kwamba anaweza kupiga dawa ya kinga kipindi ambacho mzabibu ushaingia ugonjwa au anaweza piga dawa ya ugonjwa wakati mzabibu hauna ugonjwa huo hivyo unakuta Wakulima wengi wanaingia hasara ya madawa bila sababu.
Kitu kingine cha kuzingatia hapa ni vipimo vya dawa juu ya ugonjwa husika na ukubwa wa shamba,kwa bahati nzuri dawa nyingi siku hizi zimeandikwa kwa lugha nyepesi juu ya matumizi ya dawa hizo na vipimo vyake viko wazi kabisa. Kama umeambiwa uchanganye kilo moja kwa lita mia tatu za maji
Ugonjwa wa Kinyaushi (Dampingoff)
Ugonjwa wa Kinyaushi husababishwa na vimelea vya ukungu jamii ya (Pythium, Rhizoctoniasolani, Phytophthoraspp na Sclerotium). Ukungu huu au vimelea vya ukungu wa aina hii huishi kwenye udongo.
Mimea inayoshambuliwa au kuhifadhi ugonjwa huu ni mingi mno na husababisha mnyauko wa miche ya mazao mengi shambani. Mmea uliopatwa na ugonjwa huu huwa mwembamba sanamithili ya waya hasa kwenye shina. Mara nyingine ugonjwa wa aina hii huozesha mche hata kabla ya mche kustawi vizuri.
Ugonjwa wa Ubwiri Poda (Powderymildew)
Ugonjwa huu huenea zaidi vipindi vya joto/ukame. Ugonjwa huu hushambulia zaidi mazao kama Zabibu, nyanya, hoho n.k. Majani huwa na madoadoa ya njano ambayo huambatana na poda nyeupe chini ya jani.
Namna majani ya mizabibu yalivyoathiriwa na fangasi,namna poda nyeupe inavyoonekana katika picha
Ukungu wa kuchelewa(Lateblight)
Huu ni ugonjwa wa Zabibu pia ambao kama haukudhibitiwa husababisha madhara kiasi cha karibu asilimia 90-100 ya mavuno. Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vya ukungu jamii ya Phytophthorainfestans ambayo hutokea zaidi vipindi vya baridi kali na mvua.
Hayo ni baadhi tu magonjwa ya fangasi, orodha ni ndefu kidogo. Tutajitahidi kuchagua yenye athari kubwa na yanayoshambulia mazao mengi.
Namna ugonjwa huu unavyoweza kuleta madhara kwenye matunda ya mzabibu
Jinsi ya kupambana na magonjwa ya fangasi:
1. Hakikisha unatembelea shamba lako mara 3 hadi 4 kwa wiki, au ikiwezekana kila siku. Unatakiwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara, hakikisha unazunguka shambani, kagua mimea yako kwenye majani juu na chini pamoja na shina. Uchunguzi wa mara kwa mara utasaidia kujua kwa haraka dalili za ugonjwa kabla ya kuleta madhara.
2. Hakikisha usafi wa shamba lako kuanzia wakati wa upandaji hadi baada ya kuvuna. Hakikisha palizi inafanyika kwa wakati, maana baadhi ya magugu hutumika kama mazalia ya vimelea vya fangasi, pia magugu shambani husababisha unyevunyevu ambao hustawisha fangasi. Na si hivyo tu magugu pia
huficha wadudu ambao ni waharibifu kwa mimea lakini pia wadudu hao hutumika kusambaza magonjwa hayo ya fangasi
3. Piga dawa kwa wakati hasa katika kipindi cha masika,na hakikisha unatumia dawa sahihi. Mbali na magonjwa hayo ya fangasi pia kuna magonjwa yanayosababishwa na wadudu, kama nzi,mbung’o,funza wa vitumba n.k
Kubaini mapema mayai au funza kabla hayajatoboa matunda ni muhimu sana. Funza wachanga kwanza hula majani baadae matunda. Funza wakishaingia ndani ya matunda husababisha uharibifu mkubwa. Uharibifu kwenye matunda machanga husababisha kupukutika kwake, wakati mashambulizi ya matunda yaliyokomaa husababisha matundu ambayo huruhusu kuingia kwa aina nyingine za ukungu na bakteria ambao huleta madhara zaidi.
Namna ambayo funza hawa wanaweza kuharibu mmea na matunda ya zabibu
Kemikali: Mara nyingi kemikali inayodumu kwa muda mfupi ndio inayohitajika kwani matunda hushambuliwa muda mfupi kabla ya kuvuna.
Kwa hivyo, kemikali kama vile mevinphos na endosulfan zinashauriwa kutumika. Kemikali nyingine zilizosajiliwa kutumika kwa mdudu huyu ni carbaryl, tetrachlorvinphos, methomyl, acephate, monocrotophos na dawa zenye pareto.
Hayo ni baadhi tu ya magonjwa yanayoshambulia Zabibu,ila yapo mengi sana,mpaka wataalam waliamua kuandika kitabu kinachohusu magonjwa tu ya mizabibu,kwa kuwa ndio kiini cha mkulima kuweza kupata mazao mengi kama ataweza kukabilina na magonjwa hayo.
11. Baada ya Zabibu kutoa matunda, kinachofuata ni uvunaji wa Zabibu, katika kipindi kuna hatua kama mkulima inabidi uzitilie mkazo kabla ya kuanza uvunaji, kama kuangalia kiwango cha sukari,ukubwa wa matunda, rangi ya matunda n.k. kwa mzabibu mpya inachukua miezi nane ndio huanza kuzaa japo mzao wa kwanza unakua hafifu, inapofikia miaka mitatu ndipo uzao wake huongezeka maradufu, hivyo kwa anae anza kilimo hiki asije kukata tama kwa kupata mazao machache kwa uzao wa kwanza.
Vifaa vinavyohitajika kwa uvunaji ni mikasi,kisu,kreti/ndoo, japo nimeona Wakulima wengi wakitumia viwembe kitu ambacho hatushauri kwa kuwa ni hatari hata kwa mvunaji mwenyewe.
Mkasi kwa ajili ya uvunaji namna ya kukata Zabibu bila kusababisha uharibifu
Muda wa mzuri wa kuvuna Zabibu ni asubuhi kwa kuwa muda huu jua linakua sio kali,hivyo itasaidia kupunguza matunda mengi kuanguka chini wakati wauvunaji,na pia mvunaji atakua akivuna kwa utaratibu bila kero yoyote ya jua.
Tunashauri wakati kuvuna mtu avune mstari kwa mstari na sio kuvuna hovyo hovyo,ukivuna kwa mstari itasaidia kujua unapoelekea bila kuacha Zabibu zingine shambani,mtu akivuna bila kufuata mstari anaweza kuacha baadhi ya sehemu hazijavunwa kwa kua hajui alianzia wapi na anaelekea wapi,pia atatumia muda mwingi shambani.
Namna watu wanavyovuna kwa mstari,hii inasaidia kuvuna Zabibu yote bila kuacha hata moja shambani
MWISHO
Kama nilivyoeleza hapo awali kijitabu hiki sio cha mtaala wa kilimo (academic), bali ni muongozo wa kumuwezesha mkulima wa Zabibu katika kufikia malengo yake hasa kuinua kipato chake kupitia kilimo hiki cha Zabibu.
Nilibahatika kutembelea baadhi ya Wakulima na mashamba yao nikaona kuwa kwa asilimia kubwa Wakulima wengi hawalimi kibiashara kilimo hiki bali wanalima ili wapate pesa ya kujikimu tu kama kula na kuvaa basi, nasema hivi kwa kuwa Wakulima wengi hawatunzi kumbukumbu gharama walizoingia katika kulihudumia shamba lake hivyo pia inakua ngumu kujua kama wanapata faida kiasi gani.
Kitu kingine Wakulima wengi hawawekezi katika mashamba haya,kilimo cha Zabibu ni cha gharama,na ili upate faida kubwa inakubdi uwekeze vya kutosha na sio vinginevyo. Ni bora mkulima akawekeza nguvu nyingi katika ekari moja akapata mazao mengi na sio ekari nyingi ambazo zitamshinda kuzihudumia na kusababisha apate mazao machache.
Nitoe rai kwa Wakulima waliopo na wanaotaka kuingia katika kilimo hiki wapiti muongozo huu kwa umakini,na hatua ambazo nimezieleza hapo juu wazipitie zote kwa umakini na wazihamishie kwenye vitendo nimatumaini yangu watafidika.
ASANTENI
===
MICHANGO YA WADAU KUHUSU KILIMO HIKI
MUONGOZO WA KILIMO CHA ZABIBU KIBIASHA
UTANGULIZI
Kitabu hiki kinatoa muongozo wa mbinu bora za uzalishaji wa Zabibu kwa mkulima wa kawaida,pia tumetumia lugha rahisi ili kumuwezesha mkulima kuelewa kwa urahisi,na pia kimetumia michoro mingi ili kumsaidia mkulima kuona kwa vitendo,na pia kimetumia mazingira halisi ya Wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma.
Jitihada nyingi zimefanyika ili kuhakikisha Wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma wanalima kisasa zaidi ili kujihakikishia mavuno bora na ya uhakika kipindi cha msimu wa mavuno.Kutokana na utafiti uliofanyika na Taasisi mbalimbali inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya Wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma wanalima kutumia uzoefu tu na si kitaalamu kama inavyotakiwa,hii inapelekea Wakulima wengi kutumia gharama kubwa katika uzalishaji wa zao hili kwa kuwa wengi wao wanatumia uzoefu na siutaalamu,hivyo kupelekea Wakulima kupata kipato kidogo ambacho hakilingani na uwekezezaji walioweka.
Hivyo kitabu hiki kitaainisha mbinu zote za msingi katika uzalishaji wa Zabibu ili kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji,na pia kuendesha kilimo kibiashara zaidi.
Nimatumaini yangu kuwa kama Wakulima watazifuata mbinu hizi wataongeza uzalishaji wa zao hili na hivyo kuwaongezea kipato zaidi.
SURA YA KWANZA 1:0 HISTORIA YA KILIMO CHA ZABIBU KWA UFUPI
Kilimo cha Zabibu mkoani Dodoma kina historia ndefu, ambapo kwenye miaka ya 1950 na mwaka 1974 chini ya uzaidizi wa bihwana misheni, serikali ya Tanzania wakati huo ikishirikiana na serikali ya china ilianzisha kituo cha kilimo cha Bihawana Farmers Training Center (BFTC) kwa ajili ya kufundisha Wakulima juu ya kilimo cha Zabibu na mazao mengine. Wakulima wengi walijifunza mbinu mbalimbali juu ya kilimo cha Zabibu na wengi wao walianzisha mashamba ya Zabibu. Na katika miaka ya 1990 kilianzishwa kiwanda cha mvinyo cha DOWICO,kiwanda hiki kilisababisha Wakulima wengi waingie kwenye kilimo cha Zabibu.
Katika miaka hiyo ya 1990 viwanda vya mvinyo viliongezeka na Wakulima wengi wakaanza kuanzisha mashamba ya Zabibu ili kuvilisha viwanda hivyo,.
Dodoma ndio mkoa pekee unaolima Zabibu kwa wingi nchini Tanzania na hata kwa afrika mashariki ndio mkoa wenye utajiri mkubwa wa zao hili.Hii pekee ni fursa kwa wananchi wa Dodoma katika kulitilia mkazo zao hili ili liweze kuinua uchumi wa wananchi wa mkoa huu.
Kijitabu hiki cha kilimo bora cha Zabibu kimeeleza kwa undani juu ya mbinu zote za kilimo cha Zabibu kuanzia kujua aina ya udongo,uandaaji wa shamba,maji,magonjwa,uvunaji,aina za Zabibu n.k napia kimeangazia muelekeo wa kilimo cha Zabibu kibiashara zaidi.
1:1 Ukweli kuhusu kilimo cha Zabibu
Katika kiini chake kilimo ni utatuzi wa changamoto mbalimbali,kwahiyo kama hutajiweka kama mtatuzi wa changamoto hizo ni bora uachane na kilimo. Kila siku shamba la Zabibu litakuletea changamoto mbali mbali ambazo itakubidi uzikabili,Je unaweza?kipindi cha mvua kukabiliana na magugu,unaweza ukapalilia leo baada ya siku tatu yakaota mengine,halikadhalika kipindi cha mavuno kinapokaribia kuna changamoto ya ndege wanaokuja kuharibu Zabibu na hao pia unabidi ukabiliane nao,Je uko tayari?
Nimejaribu kukuelezea haya sio kwamba nataka nikuogopeshe la hasha!ila ni kukuweka katika picha ambayo itakusaidia kujua hali halisi ya kujua majukumu utakayoenda kukabiliana nayo pindi utakapoingia katika kilimo hiki.
Swali la msingi hapa ni kwa namna gani utalima Zabibu katika vipindi vyote vya masika,kiangazi n.k katika vipindi vyote hivi kuna magonjwa kulingana na hali ya hewa ya kipindi husika.
SURA YA PILI
1.1 Maeneo yanayolimwa Zabibu mkoani Dodoma
Hali ya hewa ya Dodoma inaruhusu zao hili kustawi katika maeneo mengi mkoani hapa,baadhi ya maeneo yanayolimwa Zabibu ni Mpunguzi, Mbabala, Hombolo, Chamwino, Bahi, Mvumi, Msalato, Gawaye .
Kwa asilimia kubwa maeneo haya yanategemea mvua na kwa baadhi ya maeneo wanatumia mifumo mbalimbali ya umwagiliaji mfano Hombolo wanatumia mifereji inayopitisha maji kutoka bwawa la Hombolo,Chamwino wanatumia umwagiliaji wa matone.
Ramani ya mkoa wa Dodoma: uzalishaji mkubwa unafanywa katika wilaya ya Dodoma mjini, ikifuatiwa na chamwino na Bahi.
SURA YA TATU
3.0 HATUA KUMI ZA KUANGALIA KABLA HUJAANZISHA SHAMBA LA ZABIBU
Kumekua na wimbi kubwa kwa watu wanaofanya kazi za maofisini kuingia kwenye kilimo hiki hasa wakijua kua kilimo hiki kina tija katika kujikwamua kiuchumi,nah ii imepelekea hata wale Wakulima wazoefu na wenyewe kuongeza mashamba yao,huku wakiamini kuwa ipo siku zao hili litarudisha Heshima yake ya miaka ya tisini,kwakua sasa Zabibu inalimwa na watu wa kada tofauti tofauti. Hivyo basi kabla hujaamua kuingia kwenye kilimo hiki au kupanua shamba lako hebu jaribu kupitia hatua hizi ndipo ufanye maamuzi sahihi.
1
Kwanza unatakiwa uangalie kuwa unalenga soko lipi, je ni kwa wenye viwanda? Au wanunuzi wadogo wadogo?kama ni kwa wenye viwanda inabidi ujaribu kuongea nao kwanza uone mtazamo wao na ni aina ipi ya Zabibu wanazihitaji. Ni wazo zuri pia kama utapata mawasiliano ya uhakika na wenye viwanda ikibidi kama watakuhakikishia kuingia mkataba nao mara utakapoanza uzalishaji.
2
Pili inabidi ujue nini unakifanya,hapa namaanisha ujuzi wa zao hili, wengi wa Wakulima wanaolima zao hili kwasasa hawana utaalamu wengi wao wanatumia uzoefu tu. Sisemi kwamba wanafanya vibaya ni kitu kizuri kutumia uzoefu lakini ukiongeza na ujuzi kidogo inakua ni kitu kizuri zaidi, maana utajua nini unafanya katika kilimo hiki.
3
Tatu fanya utafiti binafsi kwa kuongea na Wakulima wazoefu ili kujua ni aina gani ya Zabibu inastawi katika eneo husika, pia kuna mabwana shamba ambao wana utalaamu juu ya kilimo hiki cha Zabibu nenda kaongee nao uone wanakushauri nini. Pia ni vyema ukazalisha Zabibu ambazo wenye viwanda vya mvinyo wanazihitaji wao ni soko la uhakika.
4
Nne kama mipango pia nikuanzisha kiwanda cha mvinyo ili Zabibu utakazolima uzipeleke kiwandani kwako. Nivyema ukafanya utafiti juu ya Masoko ya mvinyo utakaotengeneza,ujue wateja wako ni kina nani wanapendelea mvinyo wa aina gani n.k
5
Uwe na mtaji wa kutosha utakaokuwezesha kuishi kwa miaka mitatu hadi mitano bila kutegemea kipato chochote kutoka kwenye shamba lako la Zabibu, maana Zabibu itaanza kukulipa kuanzia mwaka wa tatu na kuendelea.
6
sita hakikisha unaanzisha shamba kwenye udongo sahihi unaoendana na uzalishaji wa Zabibu, udongo ndio kitu cha msingi kabisa kuzingatia kabla hujaamua kuanzisha shamba la Zabibu.
7
Saba anza na ekari chache hii itakusaidia uendelee kujifunza taratibu juu ya kilimo hiki kwa vitendo huku akili yako ikiwa imetulia,usianze na uwekezaji mkubwa maana utakupa changamoto kwa kuwa ndio mara yako ya kwanza kuanza kilimo hiki.
8
Nane, tafuta mkulima mzuri na mzoefu mwenye shamba zuri la Zabibu, au jiunge na vyama vya Wakulima wa Zabibu kama UWAZAMAM,MBABALA,GAWAYE N.K hapa utapata fursa ya kujifunza kwa vitendo namna wenzio wanavyolima Zabibu na namna wanavyokabiliana na changamoto mbalimbali za zao hili.
9
Jaribu kujifunza namna bora ya ukatiaji wa Zabibu,katika kilimo hiki cha Zabibu ukatiaji ndio kiini cha uzao wa Zabibu,ukikosea katika ukatiaji unaweza usipate mazao kwa msimu mzima. Hivyo ni muhimu ukajifunza namna bora ya ukatiaji wa mizabibu. Utaelewa kwa kina juu ya ukatiaji katika sura zinazofuata za kitabu hiki.
10
Kumi ,uwe na mtazamo wa kulima kibiashara zaidi, usilime Zabibu kwa mazoea,lima zao hili huku ukiamini kuwa hii ni kazi yako usilime kama kazi ya ziada tu. Ongeza juhudi na maarifa katika kilimo hiki.
Nimeamua kukuwekea hatua hizo kumi za kufuata kabla hujaanzisha shamba la Zabibu,hata kama tayari umeanzisha shamba la Zabibu jaribu kuzipitia hatua hizo uone kama ulizipitia au la,japo nimatumaini yangu kuwa kuna baadhi walizipitia hata kama sio zote.
3:1 AINA YA ZABIBU
Kwa ujumla kuna aina tatu za Zabibu ambazo ni Zabibu za mvinyo,Zabibu za mezani na Zabibu za kukausha ambazo zote zinazalishwa mkoani hapa. Zabibu zinazozalishwa kwa wingi mkoani hapa ni mvinyo zikifuatiwa na za mezani.
Aina zote hizo nilizozitaja hapo juu zimegawanyika katika makundi tofauti tofauti mfano Zabibu za mvinyo zimegawanyika katika makundi mawili ambapo kuna Zabibu nyekundu maalumu kwa ajili ya kutengenezea mvinyo mwekundu na kuna Zabibu nyeupe kwa ajili ya kutengenezea mvinyo mweupe.
3:2 HALI YA HEWA
Zabibu haihitaji mvua nyingi, maeneo yenye mvua za wastani ndio yanafaa kwa kilimo cha Zabibu mfano Dodoma, unaweza ukajiuliza kwanini Dodoma ni pakame lakini ndio wazalishaji wakubwa wazabibu Afrika mashariki! Pia ardhi ya Dodoma ina hifadhi maji kwa kipindi kirefu mfano kwa mvua zinazonyesha kuanzia Desemba mpaka Machi zinatosha kabisa kuhudumia mizabibu mpaka mwezi wa Julai kwa mavuno ya kiangazi.
Hali hii ya Dodoma ndio inayofanya Zabibu yake kuwa bora kuliko sehemu yoyote ile Afrika Mashariki,zina kiwango kikubwa cha sukari, pia unaweza ukazihifadhi kwa muda mrefu kidogo,zina ganda gumu ukilinganisha na Zabibu za sehem nyingine.
HATUA ZA KUFUATA WAKATI WA UANZISHWAJI WA SHAMBA LA ZABIBU
Kabla ya kuanzisha shamba la Zabibu kuna hatua kumi za msingi za kuzifuata kwa mpangilio,ili kuweza kuleta tija katika uzalishaji wa Zabibu.
1
Kufanya utafiti juu ya aina ya udongo unaofaa katika uzalishaji wa Zabibu, katika utafiti niliofanya nimegundua Wakulima wengi hawafanyi utafiti juu ya udongo unaotakiwa katika uzalishaji wa Zabibu. Udongo unaofaa kwa kilimo cha Zabibu kwa hali ya hewa ya Dodoma ni mchanganyiko wa mfinyanzi,kichanga na tifutifu,hata kama utapata mahali ambapo udongo huu wa mchanganyiko haupatikani itabidi uchimbe mitaro na unapochanganya mbolea itabidi uchanganye na aina hizo za udongo.
Moja ya faida ya aina hiyo ya udongo ni kuwa inasaidia mizizi ya mzabibu kujitawanya kwa nafasi,na pia hewa na maji vinapata nafasi kwa urahisi.
Picha: katika picha hii utaona jinsi mizizi ya Zabibu inavyojitawanya kwa nafasi kwa kua udongo huu Ulichanganywa vizuri na hivyo kuacha nafasi kwa mizizi kujitanua kwa urahisi.
2
Kuandaa mitalo kufuatana uelekeo wa jua linapotokea,unapoandaa shamba la Zabibu inabidi mistari ya mitalo uchore kufuatana na jua linapochomoza, moja ya faida ya kuangalia uelekeo wa jua ni kwamba chakula cha mmea kinatengezwa kwa nguvu ya jua pia,hivyo inakupasa kuangalia kigezo hicho ili kuweza kupata mimea yenye afya na uwezo wa kuhimili mazao yatakayo zalishwa,Zabibu inahitaji jua la kutosha ili kuweza kuzalisha chakula cha kutosha kwa mimea yake.chimba mitalo yako na uhakikishe angalau inapata jua kwa asilimia 80.
Picha,
Mitaro ya Zabibu kufuatana na ulekeo wa jua,mashariki kwenda magharibi kufuatana na picha hii
3
Kuhakikisha unapata miche bora ya mizabibu,hapa kuna Wakulima wana vitalu vyao na kuna wengine wananunua kwa Wakulima binafsi au kwa taasisi zinazojishughulisha na Zabibu mfano Makutupora kituo cha utafiti. Miche bora ya Zabibu ndio itakayo kuwezesha kupata mazao ya uhakika mbeleni, na ndio maana tunashauri Wakulima wanunue miche bora iliyoandaliwa kitaalam.
Wakulima wengi mkoani hapa wanategemea makato ya miche kutoka kwenye mashamba yao kitu ambacho sio sahihi sana maana kunakua na mzunguko mkubwa/mrefu uzao,na pia Wakulima wengi wanashindwa kuchagua makato yenye ubora nah ii hupelekea kukosa mazao ya uhakika.
Picha namba 3, makato ya Zabibu yaliyoandaliwa katika ubora wa hali ya juu,yakisubiri kuchipua
Picha namba 4,Muonekano wa kitalu kilichoandaliwa vizuri
4
Kuanda mitalo kabla hujahamishia miche shambani,hii ni hatua muhimu na Wakulima wengi hushindwa katika hatua na kujikuta wanaharibu miche mingi shambani mara tu baada ya kuihamishia maana miche huungua kwa kuwa wanashindwa kuchanganya kwa wastani mzuri mbolea na mchanga,unashauriwa katika kila kilo moja ya ya mbolea/samadi unachanganya mchanga robo kilo,na baada ya kuchanganya unatakiwa ufukie mitaro yako kwa muda wa mwezi mmoja au miwili ili kuacha mbolea ioze vizuri na kuiacha ardhi ikiwa na rutuba ya kutosha,pia tunashauri Wakulima wanaoandaa mashamba/mitalo mipya kuiandaa kuanzia mwezi November ili mvua zitakazoanza desemba zikute umeshafukia mitalo yako vizuri na kuozesha mbolea kwa haraka zaidi.
Udongo uliochanganywa vizuri na samadi mitaro iliyoandaliwa vizuri kwa nafasi
5
Kuhamishia miche kutoka kwenye kitalu na kuhamishia kwenye shamba lililoandaliwa vizuri,usije ukahamishia miche kwenye shamba ambalo halikuandaliwa vizuri maana itakugharimu hutapata matokeo mazuri baada ya muda kupita. Kabla ya kuanza kuhamisha miche kwenye shamba inabidi uhakikishe kuna maji ya kutosha maana kila mche unatakiwa uwe kwenye unyevu ili kuzoea maisha mapya ya shambani.pia ni vyema Wakulima wazingatie nafasi kati ya mche na mche na mtaro na mtaro
Shamba liloandaliwa vizuri tayari kuhamisha miche,hapa ndipo miche hii itamalizia masiha yao hapa hivyo ni vyema eneo liandaiwe vizuri.
6
Baada ya miche ya Zabibu kuhamishiwa shambani katika hatua hii, mkulima inakupasa kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha hakuna mmea unaokufa ama kwa ukame au kuliwa na wadudu.uzoefu unaonesha kuwa Wakulima wengi wakishahamishia miche shambani wanajua washamaliza kazi,hivyo ni vyema kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kujua maendeleo ya miche yote.
Mmea wa mzabibu wenye afya nzuri na ambao unafuatiliwa kwa ukaribu sana
7
Baada ya miche kushika vizuri, itaanza kustawi na kuonesha dalili za kutambaa,hivyo basi hichi ni kipindi cha kuanza kuifundisha namna ya kutambaa kwa kutumia kamba na fito nyembamba.
Picha hizi zinaonesha ni namna gani unaweza kufundisha mmea wa Zabibu namna ya kutambaa kwenye wire na fito
8
Baada ya kuufundisha mmea wa Zabibu,kinachofuata ni ukatiaji wa mzabibu,katika hatua hii hapa ndipo unaundaa mmea wako kwa ajili ya uzao,bila kukatia huwezi kupata mazao.vifaa vinavyotumika kwa ukatiaji ni kama mkasi,msumeno n.k..kuna aina mbili za ukatiaji wa mizabibu ambapo kuna Dodoma cordon ambao utakuwezesha kupata mazao kwa misimu miwili,na southAfrican type of pruning (ukatiaji wa kia Afrika kusini) ambao utakuwezesha kupata mazao kwa msimu mmoja.
Vifaa vya ukatiaji
namna ya ukatiaji
9
Hatua inayofuata ni uzaaji wa mizabibu iliyokatiwa vizuri,kama ulivyoona katika hatua namba nane kuwa ukatiaji ndio unaosababisha mzabibu kuzaa,na pia ubora wa matunda.
Hatua inazopitia mmea wa mzabibu toka kukatiwa mpaka kuzaa matunda yenye ubora
10
moja ya mambo ambayo yamekua ni changamoto kubwa wakulima wengi ni Wadudu na magonjwa ya mizabibu. Magonjwa pamoja na wadudu waharibifu wanaweza kuchangia kupata hasara hadi ya asilimia 100. Baada ya kuandaa shamba, kununua miche na kupanda miche yako, kazi kubwa inakua ni utunzaji wa mizabibu yako. zabibu ni moja ya mazao yanayopendelewa sana na wadudu na magonjwa, hivyo inahitajika umakini wa hali ya juu sana. Kwanza tunachotakiwa kufahamu ni kwamba Zabibu inahitaji ufuatiliaji wa karibu sana.
Kuna vitu viwili hapa naomba nivieweke sawa
unashauriwa ufanye hivyo au kama umeambiwa lita moja ni kwa shamba la ekari moja basi huna budi kufanya hivyo na si vinginevyo. Kuzidisha dozi au kupunguza dozi haitakiwi katika kilimo hiki.
- Kuna kinga dhidi ya mzabibu –ambapo kuna dawa kwa ajili ya kinga
- Kuna kutibu mzabibu baada ya kupata ugonjwa-kuna dawa zake pia
Kitu ambacho Wakulima wengi hawafuatilii ni kwamba anaweza kupiga dawa ya kinga kipindi ambacho mzabibu ushaingia ugonjwa au anaweza piga dawa ya ugonjwa wakati mzabibu hauna ugonjwa huo hivyo unakuta Wakulima wengi wanaingia hasara ya madawa bila sababu.
Kitu kingine cha kuzingatia hapa ni vipimo vya dawa juu ya ugonjwa husika na ukubwa wa shamba,kwa bahati nzuri dawa nyingi siku hizi zimeandikwa kwa lugha nyepesi juu ya matumizi ya dawa hizo na vipimo vyake viko wazi kabisa. Kama umeambiwa uchanganye kilo moja kwa lita mia tatu za maji
Ugonjwa wa Kinyaushi (Dampingoff)
Ugonjwa waKinyaushi husababishwa na vimelea vya ukungu jamii ya (Pythium, Rhizoctoniasolani,
Phytophthoraspp na Sclerotium). Ukungu huu au vimelea vya ukungu wa aina hii huishi kwenye udongo.
Mimea inayo shambuliwa au kuhifadhi ugonjwa huu ni mingi mno na husababisha mnyauko wa miche ya
mazao mengi shambani. Mmea uliopatwa na ugonjwa huu huwa mwembamba sanamithili ya waya hasa
kwenye shina. Mara nyingine ugonjwa wa aina hii huozesha mche hata kabla ya mche kustawi vizuri.
Ugonjwa wa Ubwiri Poda (Powderymildew)
Ugonjwa huu huenea zaidi vipindi vya joto/ukame. Ugonjwa huu hushambulia zaidi mazao kama
Zabibu,nyanya,hoho n.k. Majani huwa na madoadoa ya njano ambayo huambatana na poda nyeupe chini
ya jani.
Namna majani ya mizabibu yalivyoathiriwa na fangasi,namna poda nyeupe inavyoonekana katika picha
Ukungu wa kuchelewa(Lateblight)
Huu ni ugonjwa wa Zabibu pia ambao kama haukudhibitiwa husababisha madhara kiasi cha karibu
asilimia 90-100 ya mavuno. Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vya ukungu jamii
ya Phytophthorainfestans ambayo hutokea zaidi vipindi vya baridi kali na mvua.
Hayo ni baadhi tu magonjwa ya fangasi, orodha ni ndefu kidogo. Tutajitahidi kuchagua yenye athari
kubwa na yanayoshambulia mazao mengi.
Namna ugonjwa huu unavyoweza kuleta maadhara kwenye matunda ya mzabibu
Jinsi ya kupambana na magonjwa ya fangasi:
1. Hakikisha unatembelea shamba lako mara 3 hadi 4 kwa wiki, au ikiwezekana kila siku. Unatakiwa
kufanya ukaguzi wa mara kwa mara, hakikisha unazunguka shambani, kagua mimea yako kwenye
majani juu na chini pamoja na shina. Uchunguzi wa mara kwa mara utasaidia kujua kwa haraka dalili za
ugonjwa kabla ya kuleta madhara.
2. Hakikisha usafi wa shamba lako kuanzia wakati wa upandaji hadi baada ya kuvuna. Hakikisha palizi
inafanyika kwa wakati, maana baadhi ya magugu hutumika kama mazalia ya vimelea vya fangasi, pia
magugu shambani husababisha unyevunyevu ambao hustawisha fangasi. Na si hivyo tu magugu pia
huficha wadudu ambao ni waharibifu kwa mimea lakini pia wadudu hao hutumika kusambaza magonjwa
hayo ya fangasi
3. Piga dawa kwa wakati hasa katika kipindi cha masika,na hakikisha unatumia dawa sahihi
Mbali na magonjwa hayo ya fangasi pia kuna magonjwa yanayosababishwa na wadudu, kama nzi,mbung’o,funza wa vitumba n.k
kubaini mapema mayai au funza kabla hayajatoboa matunda ni muhimu sana. Funza wachanga kwanza hula majani baadae matunda. Funza wakishaingia ndani ya matunda husababisha uharibifu mkubwa. Uharibifu kwenye matunda machanga husababisha kupukutika kwake, wakati mashambulizi ya matunda yaliyokomaa husababisha matundu ambayo huruhusu kuingia kwa aina nyingine za ukungu na bakteria ambao huleta madhara zaidi.
Namna ambayo funza hawa wanaweza kuharibu mmea na matunda ya zabibu
Kemikali: Mara nyingi kemikali inayodumu kwa muda mfupi ndio inayohitajika kwani matunda hushambuliwa muda mfupi kabla ya kuvuna. Kwa hivyo, kemikali kama vile mevinphos na endosulfan zinashauriwa kutumika. Kemikali nyingine zilizosajiliwa kutumika kwa mdudu huyu ni carbaryl, tetrachlorvinphos, methomyl, acephate, monocrotophos na dawa zenye pareto.
Hayo ni baadhi tu ya magonjwa yanayoshambulia Zabibu,ila yapo mengi sana,mpaka wataalam waliamua kuandika kitabu kinachohusu magonjwa tu ya mizabibu,kwa kuwa ndio kiini cha mkulima kuweza kupata mazao mengi kama ataweza kukabilina na magonjwa hayo.
11
Baada ya Zabibu kutoa matunda, kinachofuata ni uvunaji wa Zabibu,katika kipindi kuna hatua kama mkulima inabidi uzitilie mkazo kabla ya kuanza uvunaji,kama kuangalia kiwango cha sukari,ukubwa wa matunda,rangi ya matunda n.k. kwa mzabibu mpya inachukua miezi nane ndio huanza kuzaa japo mzao wa kwanza unakua hafifu,inapofikia miaka mitatu ndipo uzao wake huongezeka maradufu,hivyo kwa anae anza kilimo hiki asije kukata tama kwa kupata mazao machache kwa uzao wa kwanza.
Vifaa vinavyohitajika kwa uvunaji ni mikasi,kisu,kreti/ndoo, japo nimeona Wakulima wengi wakitumia viwembe kitu ambacho hatushauri kwa kuwa ni hatari hata kwa mvunaji mwenyewe.
Mkasi kwa ajili ya uvunaji namna ya kukata Zabibu bila kusababisha uharibifu
Muda wa mzuri wa kuvuna Zabibu ni asubuhi kwa kuwa muda huu jua linakua sio kali,hivyo itasaidia kupunguza matunda mengi kuanguka chini wakati wauvunaji,na pia mvunaji atakua akivuna kwa utaratibu bila kero yoyote ya jua. Tunashauri wakati kuvuna mtu avune mstari kwa mstari na sio kuvuna hovyo hovyo,ukivuna kwa mstari itasaidia kujua unapoelekea bila kuacha Zabibu zingine shambani,mtu akivuna bila kufuata mstari anaweza kuacha baadhi ya sehemu hazijavunwa kwa kua hajui alianzia wapi na anaelekea wapi,pia atatumia muda mwingi shambani.
Namna watu wanavyovuna kwa mstari,hii inasaidia kuvuna Zabibu yote bila kuacha hata moja shambani
MWISHO
Kama nilivyo eleza hapo awali kijitabu hiki sio cha mtaala wa kilimo (academic), bali ni muongozo wa kumuwezesha mkulima wa Zabibu katika kufikia malengo yake hasa kuinua kipato chake kupitia kilimo hiki cha Zabibu. Nilibahatika kutembelea baadhi ya Wakulima na mashamba yao nikaona kuwa kwa asilimia kubwa Wakulima wengi hawalimi kibiashara kilimo hiki bali wanalima ili wapate pesa ya kujikimu tu kama kula na kuvaa basi, nasema hivi kwa kuwa Wakulima wengi hawatunzi kumbukumbu gharama walizoingia katika kulihudumia shamba lake hivyo pia inakua ngumu kujua kama wanapata faida kiasi gani. Kitu kingine Wakulima wengi hawawekezi katika mashamba haya,kilimo cha Zabibu ni cha gharama,na ili upate faida kubwa inakubdi uwekeze vya kutosha na sio vinginevyo. Ni bora mkulima akawekeza nguvu nyingi katika ekari moja akapata mazao mengi na sio ekari nyingi ambazo zitamshinda kuzihudumia na kusababisha apate mazao machache.