Msaada kipimo cha damu ESD 120 kina maanisha nini??

Jasnira

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
608
Reaction score
382
Msaada kipimo cha damu ESD 120 ni tatizo gani
 
Angalia vizuri, ni ESD au ESR? nafikiri itakuwa ESR na sio ESD, angalia vizuri utupe feedback
 
Labda ndio hyo ESR 120 kikiwa 120 ndio nini??
 
inaonyesha kuna inflammation lakini hiki kipimo sio specific, huwa kinatumika kusupport diagnosis. daktari aliyeagiza kifanyike anatakiwa akueleze zaidi.
Kwa kifupi hakiwezi kusema una ugonjwa gani
 
inaonyesha kuna inflammation lakini hiki kipimo sio specific, huwa kinatumika kusupport diagnosis. daktari aliyeagiza kifanyike anatakiwa akueleze zaidi.
Kwa kifupi hakiwezi kusema una ugonjwa gani
Lakini ESR 120 mm/hr bado ni juu sana i.e. zaidi ya mara 10 ya kawaida.
 
George ni mtoto ana miaka 7 anapata majipu na mba tumempeleka hospital wakawa hawana physician wakutupa ufanunuzi 120 mm/ hr nimeshindwa kuelewa ni nini..?
 
Lakini ESR 120 mm/hr bado ni juu sana i.e. zaidi ya mara 10 ya kawaida.
ni kweli kipo juu sana, lakini hatuwezi sema ana ugonjwa gani, labda atueleze ana shida gani. huenda daktari aliorder ESR ili ajiridhishe na diagnosis yake
 
How serious it is?? Maelezo zaidi plz nipo njia panda
 
How serious it is?? Maelezo zaidi plz nipo njia panda

Umesema anapata majipu na mba..hii ndio inasababisha hiyo ESR kuwa juu, cha muhimu apate matibabu ya hayo majipu na mba, hiyo ESR itashuka.
ESR isikupe presha, sababu hata malaria inapandisha ESR.
 
Asante kop,
tumeenda hospital nyingine wamesema tuende j3 afanyiwe blood check up kwa undani zaidi

asante na George
 
Hyo hospital wamesema tutoe elfu 50 iliwafanye hyo check up maana wanasema inaweza kuwa na ugonjwa zaidi ya hayo majipu na mba
 
Hyo hospital wamesema tutoe elfu 50 iliwafanye hyo check up maana wanasema inaweza kuwa na ugonjwa zaidi ya hayo majipu na mba
kuna vipimo vya kufanya kwa kesi kama yako, haswa ni culture and sensitivity ambapo wataotesha sample watakayotoa kwenye jipu ili kujua aina ya bakteria na dawa sahihi ya kumpa pia wanaweza fanya blood culture, ambapo wataotesha damu ili kuona kama kuna bakteria kwenye damu. Vipimo hivi gharama yake ipo juu kidgo na sio kila hospital wanaweza fanya.
Cha muhimu hakikisha unaelezwa kila kinachofanyika na pia uliuliza pale usipoelewa
 
Nawaombea kwa jina la YESU Kristo BWANA awapiganie na yeye ni mwaminifu na wa haki.Ee baba wakumbatie watu hawa!AMEN
 
Umesema anapata majipu na mba..hii ndio inasababisha hiyo ESR kuwa juu, cha muhimu apate matibabu ya hayo majipu na mba, hiyo ESR itashuka.
ESR isikupe presha, sababu hata malaria inapandisha ESR.

Uko sawa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…