Msaada kisheria: Kucheleweshewa mishahara

Mlachake

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2009
Posts
4,437
Reaction score
4,618
Wandugu,
Vyuma vimekaza kweli kweli, Mhindi wangu mpaka leo hajanilipa mshahara wangu wa mwezi uliopita nahisi wa December ndio nitalipwa January mwishoni.

Hivi hakuna sheria yoyote inambana muajiri kwenye suala la kuchelewesha mishahara?

Nimeipitia labour law act karibu yote lakini naona maruweruwe
 
Pole mkuu na hii kweli inaboa sana
 
Ishu hapa ungeelez Hyo mhindi anatoa sababu gan kuhusu kuchelewa kwa mishahara?ndo tujue tunakusaidiaj?
 
Sheria ya wafanyakazi na mahusiano kazini ktk kifungu cha 27 ambacho ni mahususi kwa ajili ya malipo ya mishaara, hakija sema chochote na sheria kiujumla ipo kimya tu, ila isipokua sheria hio sura namba 366 inasisitiza muajiri alipe kama mkataba unavyosema, sasa kuchelewesha kwa muda mrefu kulipa ni moja ya sababu ya kuuvunja mkataba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…