Msaada kisheria kuhusu mirathi

Mpwa vipi kuhusu mrejesho ulipoenda kwa 'mtaalam' kuwafanyia walokuibia vifaa vya gari??? Nina hamu ya kuupata asee

Mkuu nimerudi! kuna observations lkn ni km nusu nusu, nafanya timing kdg then ntauleta hapa!
 
Habari jamani

Nataka kuanza kufwatilia mirathi ya mzazi, mim ndo msimamizi, tayar nshapata vitu muhim kama
death certificate, nilikuwa tayar na muhtasar wa kikao kilichiniteua, na kukubali nisimamie,

Ninachokosa ni mwongozo

Wapi naanza, niende na nn na nn, wapi niepuke kama mnavyojua nilivyosikia mirath inasumbua

Naomba msaada wenu
Asante
 
Ok kama mhutasar wa kikao unao ni vema.itabid utangaze kwenye gazeti la serekali.kama uhuru na mzalendo.ukitoka hapo unaenda mahakamani kwajili yakupata hati ya usmamiz lakin kama hatojtokeza mtu na pingamiz.kama atajitokeza bas ndo ligi hio yakuchelewesha
 
Ndugu yangu Kinene, kama kikao halali cha familia au ukoo kilikuchagua wewe uwe msimamizi wa mirathi ya marehemu, kinachofuatia hapo nenda mahakamani ukafungue mirathi.
kufungua mirathi mahakamani ni nini?
ni kuiomba mahakama ikuridhie na kukuteua kuwa msimamizi wa mirathi hiyo. hapa unakuwa na nguvu kisheria tofauti na ulipochaguliwa na kikao cha familia.
vitu vya kuendanavyo mahakamani ni pamoja na:
-barua toka serikali ya mtaa kuonesha mahali unapoishi
-kitambulisho chako wewe mfano cha kupigia kura
-muhtasari wa kikao cha familia au ukoo kilichokuchagua ww
-cheti cha kifo cha marehemu
Baada ya kufungua mirathi, mahakama itatoa tangazo ktk mbao mbali mbali za matangazo na gazeti, kukaribisha pingamiz toka kwa mtu yeyote anayepinga ww kuteuliwa ndani ya siku 90
zikipita siku hizo hakuna pingamiz, mahakama itaangalia kama sifa unazo na kukuteua rasmi kuwa msimamizi.
endapo kutakuwa na pingamiz kesi itasikilizwa kama inavyokuwa kes ya madai.
NB: unapaswa kuwa na sifa ya uaminifu kwa kiasi kikubwa
 
Nimeishia kutoa chozi mkuu asante ninaanza rasmi hii kazi.

Mzazi alifariki april mwaka huu je haina shida muda huo?
 
Nimeishia kutoa chozi mkuu asante ninaanza rasmi hii kazi.

Mzazi alifariki april mwaka huu je haina shida muda huo?

Kwa mujibu wa sheria ya mirathi na usimamizi wa mali ya mirathi inasema, mirathi yeyote haitafunguliwa mahakaman mpaka zipite siku saba (7) tokea kifo cha marehem.
hivyo uko ndani ya muda mkuu, kwan hata muda wa mwisho wa kufungua kesi za mirathi bado haujafika.
kila la kheri ktk kufuatilia mirathi.
 
vipi kwa kifo cha mwaka 1998 waweza kufungua kesi ya mirathi leo?Ni watoto 7wa mama tofauti,baba mdogo alijichagua kuwa msimamizi,sisi watoto wa bi mkubwa tulirithishwa kijijini na watoto wa bi mdogo mjini DSM.Kulikuwepo na kiwanja cha mzee kingine jirani na nyumba va Dar,dingi mdogo akajimegea akadai chakwake.
NINACHOKITAKA mali zigawiwe upya na serikali.
SABABU ZA KUCHELEWA
1.Wadogo zangu wa bimdogo walikuwa wadogo wanasoma kupitia kodi ya nyumba,niliona ningemchangnya bi mdogo.
2.Vitisho vya uchawi kutoka kwa ndugu.
 
Kwani sheria za Kislam sio sheria za nchi?

tunaposema sheria za nchi tunamaanisha za kiserikali kwa sababu serikali ndiyo inayotawala nchi na sio dini. hivyo sheria za kiserikali ndiyo za nchi kwa kuwa hutumiwa na watu wote bila kujali dini ama mila zao, tofauti na za kidini huwahusu watu wa imani hiyo.
kwa kukuongezea uelewa, sheria za din zinaweza kuwa za nchi kama nchi inaendeshwa kidin mfano nchi kama saudi arabia, iran nk
 
tunaposema sheria za nchi tunamaanisha
"Tunaposema sheria za nchi," mnaposema wewe na nani? Sijawahi kusikia hicho kitu kwingine kwa hiyo jiongelee wewe mwenyewe!

sheria za nchi tunamaanisha za kiserikali ... hivyo sheria za kiserikali ndiyo za nchi kwa kuwa hutumiwa na watu wote bila kujali dini ama mila zao

Sio kweli. Hizo unazoziita "sheria za nchi" hazitumiki "kwa watu wote bila kujali dini ama mila." Ingekuwa zinatumika "na watu wote bila kujali dini ama mila" basi kusingekuwa na mjadala wa dini/mila gani inatumika kabla ya kuanza shauri la mirathi.

Wewe mwenyewe ndio umeleta mjadala wa aina ya sheria inatakayoweza kufatwa, umeandika hivi:

hivyo bsi ni lazima kwanza ifahamike mirathi hiyo itagawanya kwa sheria za dini, sheria za nchi au za kimila kama haukuachwa wosia. .... kifungu cha 88 cha sheria ya usimamizi wa mirathi ....msimamizi wa mirathi ataigawa mali ya marehemu kwa warithi kwa mujibu wa sheria itakayoongoza


Kwa hiyo, hakuna sheria ya mirathi ambayo "hutumika kwa watu wote bila kujali dini au mila." Sheria za kimila na za Kiislam zimesimikwa na Bunge la nchi, unaposema sio za nchi zinakuwa za nini, za kijiji?
 
Ndugu yangu Anheuser, nikupongeze kwa changamoto uliyonipa,lkn iko hivi:
Sheria za kiislam hauwezi kuziita ni sheria za nchi bali zenyewe zinabaki kuwa sheria za dini ya kiislam, isipokuwa zinatambuliwa na mamlaka.
nikuulize kidogo, zipo sheria za nchi ya kenya, TZ,A.Kusin wanazo zao, marekani, Russia nk. sasa sheria za kiislam ni za nchi ipi?
kama kila nchi ina bunge linalotunga sheria za nchi hiyo, je ni bunge lipi hutunga sheria za kiislam?
katka nchi kuna mamlaka inayotunga sheria (bunge) na kuzifanyia marekebisho kuendana na matakwa ya nchi ndiyo maana sheria hizo huwa za nchi hiyo.
sheria za kiislam zinatokana na qur'an hivyo haziwezi kumilikiwa na nchi fulan bali humilikiwa na dini inayoamini kitabu hicho.
umeshawahi sikia bunge la TZ au nch yeyote inatunga au kufanya amendment sheria za dini?
hivyo basi kutambuliwa kwa sheria hiz hakuzifanyi kuwa sheria za nchi bali ni kwa jamii fulani au waumin wao.
pitia JALA s.11 uone applicability ya customary & islamic laws.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…