Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo huzika. kwa mfano mtu anayejifunza kuendesha gari akitaka kubadili mwendo wa gari itambidi afikirie sana kabla ya uamuzi huo, lakini
Unconscious mind ni pale mtu anapofanya jambo bila kutumia akili au kufikiri, tukilinganisha na mfano wa dereva hapo juu utaona kuwa madereva wote wazoefu wanatumia unconscious mind wakiwa wanaendesha magari.
Kwahiyo kwa kifupi naweza kusema kwamba
.
Conscious mind - Uzingativu/kufikiri wakati wa kutenda.
Unconscious mind- Kutozingatia/kutokufikiri wakati wa kutenda.
Tofauti za hayo conscious na unconscious mind zinategemea taarifa za tendo fulani zilizopo kwenye ubongo. Unconscious mind inatokea pale mtu anapokuwa kwenye sehemu au kitu ambacho ni kigeni kwake.
Tumezoea kutamka 1,2,3,4
.10 kwa harakaharaka. Lakini ni vigumu kutamka namba hizo ukianzia 10,9,8,7,6
.1 kwa harakaharaka.